16Yahweh amejidhihilisha; na kutekeleza hukumu; waovu wameangamia kwa matendo yao wenyewe. Selah
17Waovu wamekataliwa na kupelekwa kuzimu, mataifa yote yanayo msahau Mungu.
18Kwa kuwa mhitaji hata sahauliwa siku zote, wala matumaini ya wanyonge hayatapotea milele.