2kutangaza uaminifu wa agano lako wakati wa asubuhi na uaminifu wako kila usiku,
3kwa kinubi cha nyuzi kumi na kwa tuni ya kinubi.
4Kwa kuwa wewe, Yahwe, matendo yako yamenifurahisha. Nitaimba kwa furaha kwa sababu ya matendo ya mikono yako.
5Ni jinsi gani matendo yako ni makuu, Yahwe! mawazo yako ni ya kina.
6Mtu mpumbavu hawezi kuyajua, wala mjinga kuyaelewa haya:
7Wasio haki watakapochipuka kama nyasi, na hata watendao uovu watakapo stawi, bado wataangamizwa kwenye uharibifu wa milele.
8Lakini wewe, Yahwe, utatawala milele.
9Hakika, watazame adui zako, Yahwe! Hakika, watazame adui zako. Wataangamia! Wale wote watendao maovu watatawanywa.