58Kwa maana walimkasirisha kwa mahali pao pa juu na walimgadhabisha hata akawa na hasira ya wivu kwa miungu yao.
59Mungu aliposikia hili, alikasirika na alimkataa kabisa Israeli.
60Alipaacha patakatifu pa Shilo, na hema alikoishi kati ya watu.
61Aliruhusu nguvu zake kutekwa na kuutoa utukufu wake mkononi mwa adui.
62Aliukabidhi upanga watu wake, na aliukasirikia urithi wake.