1Mungu amefanya mwenyewe kujulikana katika Yuda; jina lake ni kuu katika Israeli.
2Hema yake iko salemu; makao yake yako yako Sayuni.
3Huko ndiko alivunja mishale ya upinde, ngao, upanga, na silaha zingine za vita. Selah
4Wewe unang'aa sana na huufunua utukufu wako, ushukapo kutoka milimani, ambako uliwauwa mateka.
5Wenye moyo shujaa walitekwa nyara; walilala mauti. Mashujaa wote walikuwa wanyonge.