11Wewe ulituingiza sisi kwenye wavu; uliweka mzigo mzito viunoni mwetu.
12Wewe uliwafanya watu wasafiri juu ya vichwa vyetu; tulipita motoni na majini, lakini ukatuleta mahali pa wazi palipo salama.
13Nitaingia nyumbani mwako nikiwa na sadaka ya kuteketezwa; nitakulipa viapo vyangu
14ambavyo midomo yangu iliahidi na kinywa changu kiliongea nilipokuwa katika dhiki.
15Nitakutolea sadaka ya kuteketezwa ya wanyama wanene pamoja na harufu nzuri ya kondoo waume; Nitatoa ng'ombe na mbuzi. Selah
16Njoni, msikie, ninyi nyote mnao mwabudu Mungu, nami nitatangaza yale yeye aliyoitendea roho yangu.
17Nilimlilia kwa kinywa changu, naye alipendezwa na ulimi wangu.