Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Zaburi - Zaburi 66

Zaburi 66:1-12

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Mpigieni Mungu kelele za shangwe, nchi yote;
2Imbeni utukufu wa jina lake; mzitukuze sifa zake.
3Mwambieni Mugu, “Matendo yako yanatisha kama nini! Kwa ukuu wa nguvu zako maadui zako watajisalimisha kwako.
4Nchi yote watakuabudu wewe na watakuimbia wewe; wataliimbia jina lako.” Selah
5Njoni na mtazame kazi za Mungu; yeye anatisha katika matendo yake awatendeayo wanadamu.
6Aligeuza bahari kuwa nchi kavu; wao walitembea kwa mguu juu ya mto; huko tulishangilia katika yeye.
7Yeye anatawala milele kwa nguvu zake; macho yake yanachunguza mataifa; waasi wasijivune. Selah
8Mtukuzeni Mungu, enyi watu wa mataifa yote, sauti ya sifa zake isikike.
9Yeye atuwekaye hai, naye hairuhusu miguu yetu iteleze.
10Kwa maana wewe, Mungu, umetupima sisi, wewe umetupima kama inavyopimwa fedha.
11Wewe ulituingiza sisi kwenye wavu; uliweka mzigo mzito viunoni mwetu.
12Wewe uliwafanya watu wasafiri juu ya vichwa vyetu; tulipita motoni na majini, lakini ukatuleta mahali pa wazi palipo salama.

Read Zaburi 66Zaburi 66
Compare Zaburi 66:1-12Zaburi 66:1-12