3Maana, tazama, wanasubiria uvamizini waniue. Wafanya maovu wenye nguvu hujikusanya wenyewe pamoja dhidi yangu, lakini sio kwa sababu ya makosa yangu au dhambi yangu, Yahwe.
4Wao wanajiandaa kunikimbiza ingawa sina kosa; amka unisaidie na unitazame.
5Ewe, Yahwe Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli, inika uwaadhibu mataifa yote; usiwe na huruma kwa mhalifu mwovu yeyote. Selah
6Wao wanarudi jioni, wanabweka kama mbwa na kuuzungukia mji.