5ambaye hasikilizi sauti ya waganga, haijalishi ustadi walio nao.
6Vunja meno yao midomoni mwao, Mungu; uyatoe meno ya mwana simba, Yahwe.
7Wayeyuke kama maporomoko ya maji; wafyatuapo mishale yao, iwe kama haina ncha.
8Wawe kama konokono ambaye huyeyuka na kutoweka, kama mtoto aliye zaliwa kabla ya wakati ambaye hakuona jua.
9Kabla ya vyungu vyenu kupata joto la kuungua kwa miiba, yeye ataviondosha kwa upepo mkali, miiba ya kijani yote na ile inayoungua.