1Je, ninyi watawala mnaongea haki? Mnahukumu kwa haki, ninyi watu?
2Hapana, mnafanya uovu mioyoni mwenu; munaeneza vurugu nchi yote kwa mikono yenu.
3Waovu huenenda katika upotovu hata walipokuwa tumboni; wao wanaenenda katika upotovu tangu kuzaliwa, wakiongea uongo.
4Sumu yao ni kama sumu ya nyoka; wako kama fira kiziwi azibaye masikio yake,
5ambaye hasikilizi sauti ya waganga, haijalishi ustadi walio nao.
6Vunja meno yao midomoni mwao, Mungu; uyatoe meno ya mwana simba, Yahwe.
7Wayeyuke kama maporomoko ya maji; wafyatuapo mishale yao, iwe kama haina ncha.
8Wawe kama konokono ambaye huyeyuka na kutoweka, kama mtoto aliye zaliwa kabla ya wakati ambaye hakuona jua.
9Kabla ya vyungu vyenu kupata joto la kuungua kwa miiba, yeye ataviondosha kwa upepo mkali, miiba ya kijani yote na ile inayoungua.