7Tazama, ningeenda mbali; ningekaa jangwani. Selah
8Ningefanya haraka kuja mafichoni mwako kuzikimbia dhoruba na tufani.”
9Uwaangamize, Bwana, vuruga lugha zao! Kwa maana nimeona vurugu na ugomvi katika mji.
10Mchana na usiku wao huenda kwenye kuta zake; uchafu na ufisadi uko katikati yake.
11Uovu uko katikati yake; ukandamizaji na uongo hauiachi mitaa yake.