1Uniokoe, Mungu, kwa jina lako, na kwa nguvu zako unihukumu.
2Usikie maombi yangu, Mungu; uyategee sikio maneno ya mdomo wangu.
3Kwa maana wageni wameinuka dhidi yangu, na watu wasio na huruma wanaitafuta roho yangu; nao hawakumuweka Mungu mbele yao. Selah
4Tazama, Mungu ni msaidizi wangu; Bwana ndiye anisaidiaye.
5Naye atawalipizia uovu maadui zangu; katika uaminifu wako, uwaharibu!
6Nitakutolea dhabihu kwa moyo mkunjufu; nitalishukuru jina lako, Yahwe, kwa maana ni jema.
7Kwa kuwa yeye ameniokoa katika kila shida; macho yangu yamewatazama adui zangu yakiwa na ushindi.