Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Zaburi - Zaburi 49

Zaburi 49:1-10

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Sikieni hili, ninyi watu wote; tegeni masikio, ninyi wenyeji wa dunia,
2wote walio chini na walio juu, tajiri na masikini wote pamoja.
3Mdomo wangu utazungumza hekima na tafakari ya moyo wangu itakuwa ya uelewa.
4Nitaelekeza sikio langu kwenye mfano; nitaanza mfano wangu kwa kinubi.
5Kwa nini nilazimike kuziogopa siku za uovu, wakati uovu umenizunguka kwenye visigino vyangu?
6Kwa nini niwaogope wale wanao amini katika mali zao na kujivuna kuhusu utajiri wao?
7Ni hakika kuwa hakuna yeyote atakaye muokoa ndugu yake au kumpa Mungu pesa kwa ajili yake,
8Kwa maana ukombozi wa uhai wa mtu ni gharama kubwa, na hakuna awezaye kulipa kile tunacho daiwa.
9Hakuna yeyote atakaye ishi milele ili mwili wake usioze.
10Maana yeye ataona uozo. Watu wenye hekima hufa; wajinga pia huangamia na kuacha mali zao kwa wengine.

Read Zaburi 49Zaburi 49
Compare Zaburi 49:1-10Zaburi 49:1-10