18Mioyo yetu haikukengeuka; hatua zetu hazikuiacha njia yako.
19Bali wewe umetuadhibu vikali katika mahali pa mbweha na kutufunika na uvuli wa mauti.
20Ikiwa tumelisahau jina la Mungu wetu au kueneza mikono yetu kwa Mungu mgeni,
21Mungu asingeligundua hili? Kwa maana yeye anazijua siri za moyo.
22Hakika, kwa ajili ya jina lako tutauawa siku zote; tunahesabiwa kuwa kondoo kwa ajili ya kuchinjwa.
23Bwana, amka, kwa nini unalala? Inuka, usitutupe moja kwa moja.
24Kwa nini unaficha uso wako na kusahau mateso yetu na kukandamizwa kwetu?
25Kwa maana tumeyeyushwa kwenye mavumbi; miili yetu imeshikamana na ardhi.
26Inuka utusaidie na utuokoe kwa ajili ya uaminifu wa agano lako.