15Hakika ninakungoja wewe, Yahwe; wewe utanijibu, Bwana Mungu wangu.
16Ninasema hivi ili kwamba maadui zangu wasije wakafurahia juu yangu. Ikiwa mguu wangu utateleza, watanifanyia mambo mabaya.
17Kwa kuwa niko karibu mashakani, na niko katika maumivu ya mara kwa mara.
18Ninatubu makosa yangu; ninahuzunika kwa dhambi zangu.
19Lakini maadui zangu ni wengi; wale wanichukiao ni wengi.
20Wao wananilipa mabaya kwa mema; wanavurumiza shutuma kwangu ingawa nimefuata lililo jema.
21Usinitelekeze, Yahwe, Mungu wangu, usikae mbali nami.
22Njoo haraka unisaidie, Bwana, wokovu wangu.