20Bali waovu wataangamia. Maadui wa Yahwe watakuwa kama vile utukufu wa malisho; watamalizwa na kupotezwa katika moshi.
21Mtu mwovu hukopa lakini halipi, bali mtu mwenye haki ni mkarimu na hutoa.
22Wale walio barikiwa na Mungu watairithi nchi; wale aliowalaani watafutiliwa mbali.
23Hatua za mwanadamu zinaimarishwa na Yahwe, mtu ambaye njia zake zinakubalika machoni pa Mungu.
24Ajapojikwaa, hataanguka chini, kwa kuwa Yahwe anamshikilia kwa mkono wake.
25Nilikuwa kijana na sasa ni mzee; sijawahi kumuona mtu mwenye haki ametelekezwa wala watoto wake kuombaomba mkate.
26Wakati wote yeye ni mkarimu na hukopesha, nao watoto wake hufanyika baraka.
27Acha uovu na ufanye yaliyo mema; ndipo utakapokuwa salama milele.
28Kwa maana Yahwe hupenda haki naye hawaachi wafuasi waaminifu. Wao hutunzwa milele, lakini uzao wa waovu utafutiliwa mabli.
29Wenye haki watairithi nchi na kuaa huko milele.
30Mdomo wa mwenye haki huongea hekima na huongeza haki.
31Sheria ya Mungu wake imo moyoni mwake; miguu yake haitelezi.
32Mtu mwovu humvizia mwenye haki na kutafuta kumuua.
33Yahwe hatamuacha yeye kwenye mkono wa mtu mwovu wala kumlaumu atakapohukumiwa.
34Umngoje Yahwe na uishike njia yake, naye atakuinua uimiliki nchi. Atakapo waondosha waovu wewe utaona.
35Nimewaona waovu na mtu wa kutisha akienea kama mti wa kijani katika udongo wa asili.
36Lakini nilipopita tana mara nyingine, hakuwepo pale. nilimtafuta, lakini sikumpata.
37Uwachunguze watu waadilifu, na uwatambue wenye haki; kuna hatima nzuri kwa ajili ya mtu wa amani.
38Mwenye dhambi wataharibiwa kabisa; hatima ya mtu mwovu ni kuondoshwa.
39Wokovu wa haki unatoka kwa Yahwe; yeye huwalinda wao nyakati za shida.