16Hakuna mfalme anayeokolewa na jeshi kubwa; shujaa haokolewi na nguvu zake nyingi.
17Farasi sio salama kwa ajili ya ushindi; ijapokuwa nguvu zake ni nyingi, hawezi kuokoa.
18Tazama, macho ya Yahwe yako kwa wale wanao mhofu yeye, wale wanao litumainia agano lake takatifu
19kuwaokoa maisha yao na mauti na kuwaweka hai wakati wa jaa.
20Sisi tunamngoja Yahwe, yeye ni msaada wetu na ngao yetu.
21Mioyo yetu hufurahia ndani yake, kwa kuwa tunaamini katika jina lake takatifu.