1Yahwe, ninalia; mwamba wangu, usinipuuze. Ikiwa haunijibu, nitaungana na wale waendao chini kaburini.
2Sikia kilio cha kusihi kwangu pale niitapo msaada kutoka kwako, niinuapo mikono yangu mbele ya mahali patakatifu zaidi!
3Usiniburute pamoja na waovu, wale wafanyao uovu, waongeao amani na majirani zao lakini mioyoni mwao mna uovu.
4Uwape kulingana na sitahili ya matendo yao na uwalipe kulingana na madai ya maovu yao, uwalipe kwa ajili ya kazi ya mikono yao na uwape kile wanachostahili.
5Kwa sababu hawayaelewi matendo ya Yahwe wala kazi ya mikono yake, atawakanyaga kanyaga chini na hata wajenga tena wao.
6Abarikiwe Yahwe kwa sababu yeye amesikia sauti ya kusihi kwangu!