15Siku zote macho yangu yanamtazama Yahwe, kwa kuwa yeye ataifungua miguu yangu kwenye nyavu.
16Unigeukie mimi na unihurumie; kwa maana niko peke yangu na niliye matesoni.
17Maumivu ya moyo wangu yameongezeka; uniondoe katika dhiki hii!
18Tazama mateso yangu na taabu yangu; unisamehe dhambi zangu zote.
19Ona maadui zangu, kwa maana ni wengi; wananichukia kwa chuki ya kikatili.