1Nchi ni ya Yahwe, na vyote viijazavyo, dunia, na wote wakaao ndani yake.
2Kwa kuwa yeye aliianzisha juu ya bahari na kuiimarisha juu ya mito.
3Ni nani atakaye panda mlima wa Yahwe? Ni nani atakaye simama patakatifu pake?
4Yeye ambaye ana mikono misafi na moyo safi; ambaye hajauinua uongo, na haja apa kiapo ili kudanganya.
5Yeye atapokea baraka kutoka kwa Yahwe na haki kutoka kwa Mungu wa wokovu wake.
6Kizazi cha wale wamtafutao Mungu ni kama hiki, wale ambao wanautafuta uso wa Mungu wa Yakobo.
7Inueni vichwa vyenu, ninyi malango; muinuliwe juu, milango ya milango ya kudumu, ili kwamba Mfalme wa utukufu aweze kuingia!