Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Zaburi

Zaburi 1

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Amebarikiwa mtu yule asiye enenda katika ushauri wa waovu, au kusimama katika njia ya wenye dhambi, au kukaa katika kusanyiko la wenye mizaha.
2Bali yeye huifurahia sheria ya Yahwe, na huitafakari sheria yake mchana na usiku.
3Atakuwa kama mti uliopandwa karibu na mkondo wa maji ambao huzaa matunda yake kwa majira yake, ambao majani yake hayakauki; lolote afanyalo litafanikiwa.
4Waovu hawako hivyo, wao badala yake ni kama makapi yapeperushwayo na upepo.
5Kwa hivyo waovu hawatasimama katika hukumu, wala wenye dhambi katika kusanyiko la wenye haki.
6Kwa kuwa Yahweh huikubali njia ya wenye haki, njia ya waovu itaangamizwa.