Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Mithali

Mithali 3

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Mwanangu, usizisahau amri zangu na uyatunze mafundisho yangu katika moyo wako,
2maana ziatakuongezea siku zako na miaka ya maisha yako na amani.
3Usiache utiifu wa agano na uaminifu viondoke kwako, vifunge katika shingo yako, viandike katika vibao vya moyo wako.
4Ndipo utapata kibali na heshima mbele Mungu na wanadamu.
5Mtegemee Yehova kwa moyo wako wote na wala usitegemee ufahamu wako mwenyewe,
6katika njia zako zote mkiri Yeye na yeye atayanyosha mapito yako.
7Usiwe mwenye busara machoni pako mwenyewe; mche Yehova na jiepushe na uovu.
8Itakuponya mwili wako na kukuburudisha mwili wako.
9Mheshimu Yehova kwa utajiri wako na kwa malimbuko ya mazao kwa kila unachozalisha,
10na ndipo ghala zako zitajaa na mapipa makubwa yatafurika kwa divai mpya.
11Mwanangu, usidharau kuadibishwa na Yohova na wala usichukie karipio lake,
12maana Yehova huwaadibisha wale wapendao, kama baba anavyoshughulika kwa mtoto wake ampendezaye.
13Yeye apataye hekima anafuraha, naye hupata ufahamu.
14Kwani katika hekima unapata manufaa kuliko ukibadilisha kwa fedha na faida yake inafaa zaidi kuliko dhahabu.
15Hekima inathamani zaidi kuliko kito, na hakuna unachokitamani kinaweza kulinganishwa na hekima.
16Yeye anasiku nyingi katika mkono wake wa kuume; na mkono wake wa kushoto ni utajiri na heshima.
17Njia zake ni njia za ukarimu na mapito yake ni amani.
18Yeye ni mti wa uzima kwa wale wanaomshikilia, wale wanaomshikilia wanafuraha.

19Kwa hekima Yehova aliweka msingi wa dunia, kwa ufahamu aliziimarisha mbingu.
20Kwa maarifa yake vina vilipasuka na mawingu kudondosha umande wake.
21Mwanangu, zingatia hukumu ya kweli na ufahamu, na wala usiache kuvitazama.
22Vitakuwa uzima wa nafsi yako na urembo wa hisani wa kuvaa shingoni mwako.
23Ndipo utatembea katika njia yako kwa usalama na mguu wako hautajikwaa;
24ulalapo hutaogopa; utakapolala, usingizi wako utakuwa mtamu.
25Usitishwe na hofu ya ghafula au uharibifu uliosababishwa na waovu unapotokea,
26kwa maana Yehova utakuwa upande wako na ataulinda mguu wako usinaswe kwenye mtego.
27Usizuie mema kwa wale wanaoyastahili, wakati utendaji upo ndani ya mamlaka yako.
28Jirani yako usimwambie, “Nenda, na uje tena, na kesho nitakupa,” wakati pesa unazo.
29Usiweke mpango wa kumdhuru jirani yako- anayeishi jirani nawe na yeye anakuamini.
30Usishindane na mtu pasipo sababu, ikiwa hajafanya chochote kukudhuru.
31Usimhusudu mtu jeuri au kuchagua njia zake zozote.
32Maana mtu mjanja ni chukizo kwa Yehova, bali humleta mtu mwaminifu kwenye tumaini lake.
33Laana ya Yehova ipo katika nyumba ya watu waovu, bali huibariki maskani ya watu wenye haki.
34Yeye huwadhihaki wenye dhihaka, bali huwapa hisani watu wanyenyekevu.
35Watu wenye busara huirithi heshima, bali wapumbavu huinuliwa kwa fedheha yao wenyewe.