Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Mithali

Mithali 31

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Maneno ya mfalme Lemueli - mausia aliyofundishwa na mama yake.
2Mwanangu nini? Na ni nini mwana wa tumbo langu? Na ni nini mwana wa nadhiri zangu?
3Nguvu zako usiwape wanawake; au wenye kuharibu wafalme njia zako.
4Lemueli, kunywa divai, siyo kwa ajili ya wafalme, wala kwa watawala kuuliza, “kileo kikali kiko wapi?”
5Kwa sababu kama watakunywa, watasahau sheria ni nini, na kupotosha haki za wote walioonewa.
6Wape kileo kikali watu wanaopotea na mvinyo kwa wale wenye kutaabika kwa uchungu.
7Atakunywa na kusahau umasikini wake na hataikumbuka taabu yake.
8Ongea kwa ajili yao wasioweza kuongea, kwa madai ya wote wanaopotea.
9Ongea na uhukumu kwa vipimo vya haki na utetee dai la masikini na watu wahitaji.
10Mke hodari ni nani anaweza kumpata? Thamani yake ni zaidi kuliko vito.
11Moyo wa mume wake humwamini, na hatakuwa masikini.
12Humtendea mambo mema na wala si mabaya siku zote za maisha yake.
13Huchagua sufu na kitani, na hufanya kazi yake ya mikono kwa furaha.
14Yupo kama meli za wafanyabiashara; huleta chakula chake kutoka mbali.
15Huamka wakati wa usiku na kuwapa chakula watu wa kaya yake, na kugawa kazi kwa watumishi wake wa kike.
16Hulifikiria shamba na kulinunua, kwa tunda la mikono yake hupanda shamba la mizabibu.
17Yeye mwenyewe hujivika nguvu na kuimarisha mikono yake.
18Huangalia ni kipi kitaleta faida nzuri kwake; usiku wote taa yake haizimishwi.

19Mikono yake huiweka kwenye mpini wa kisokotea nyuzi na hushikilia kisokotea nyuzi.
20Mkono wake huwafikia watu masikini; mikono yake huwafikia watu wahitaji.
21Haogopi theluji kwa ajili ya kaya yake, kwa maana nyumba yake yote imevika kwa nguo nyekundu.
22Hutengeneza matandiko ya kitanda chake, na huvaa nguo za kitani ya dhambarau safi.
23Mume wake anajulikana malangoni, anapoketi na wazee wa nchi.
24Hutengeneza mavazi ya kitani na kuyauza, na naleta mishipi kwa wafanyabiashara.
25Amevaa nguvu na heshima, na wakati ujao huucheka.
26Anafumbua kinywa chake kwa hekima na sheria ya ukarimu ipo kwenye ulimi wake.
27Huangalia njia za nyumba yake na hawezi kula mkate wa uvivu.
28Watoto wake huinuka na kumwita heri na mume wake humsifia, akisema,
29“Wanawake wengi wamefanya vizuri, lakini wewe umewapita wote.”
30Madaha ni udanganyifu, uzuri ni ubatili; bali mwanamke amchaye Yehova, atasifiwa.
31Mpeni tunda la mikono yake na kazi zake zimsifu katika malango.