Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Mithali

Mithali 6

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Mwanangu, kama utaweka pesa zako kuwa dhamana kwa mkopo wa jirani yako; kama ukitoa ahadi yako katika mkopo wa mtu usiyemjua,
2basi umejiwekea mtego mwenyewe na umenaswa kwa maneno ya kinywa chako.
3Mwanagu, ukinaswa kwa maneno yako mwenyewe, fanya haya ili kujiokoa, kwa kuwa umeangukia kwenye mikono ya jirani yako; nenda unyenyekee na ufanye shauri mbele ya jirani yako.
4Usiruhusu usingizi katika macho yako wala kope za macho yako kusinzia.
5Jiokoe mwenyewe kama swala kutoka katika mkono wa mwindaji, kama ndege kutoka katika mkono wa mwinda ndege.
6Wewe mtu mvivu, mwangalie mchwa, zitafakari njia zake ili kupata busara.
7Hana akida, afisa au mtawala,
8lakini huandaa chakula chake wakati wa joto na wakati wa mavuno huweka hazina ili kula baadaye.
9Ewe mtu mvivu, utalala hata lini? Wakati gani utainuka usingizini?”
10Lala kidogo, sizia kidogo, kunja mikono kupumzika kidogo” -
11ndipo umasikini wako utakapokujia kama mporaji na uhitaji wako kama askari wa vita.
12Mtu asiyefaa-mtu mwovu- huishi kwa kauli za udanganyifu wake,
13akipepesa macho yake, akiashilia kwa miguu yake na kusonta kwa videle vyake.
14Hufanya njama za uovu kwa hila ya moyo wake; daima huchochea faraka.
15Kwa hiyo msiba wake utamkumba kwa ghafula, punde atavunjika vibaya wala hatapona.
16Kuna vitu sita ambavyo Yehova huvichukia, saba ambavyo ni chukizo kwake.
17Macho ya mtu mwenye kiburi, ulimi wa uongo, mikono inayomwaga damu ya watu maasumu,
18moyo unaobuni njama mbaya, miguu inayokimbilia maovu upesi,

19shahidi asemaye uongo na apandaye faraka kati ya ndugu.
20Mwanangu, itii amri ya baba yako na wala usiyaache mafundisho ya mama yako.
21Uyafunge katika moyo wako siku zote; yafunge kwenye shingo yako.
22utembeapo, yatakuongoza; ulalapo yatakulinda, na uamkapo yatakufundisha.
23Maana amri ni taa, na mafundisho ni nuru; kinga za kuadilisha za njia ya uzima.
24Yanakulinda dhidi ya mwanamke malaya, dhidi ya maneno laini ya uzinzi.
25Moyoni mwako usiutamani uzuri wake wala usitekwe katika kope zake.
26Kulala na malaya inaweza kugharimu bei ya kipande cha mkate, lakini mke wa mtu mwingine inagharimu uzima wako wote.
27Je mtu anaweza kubeba moto katika kifua chake bila kuuguza mavazi yake?
28Je mtu anaweza kutembea juu ya makaa bila kuchomwa miguu yake?
29Ndivyo alivyo mtu alalaye na mke wa jirani yake; yule alalaye na huyo mke hatakosa adhabu.
30Watu hawawezi kumdharau mwizi kama anaiba ili kukidhi hitaji lake la njaa.
31Walakini akimatwa, atalipa mara saba ya kile alichoiba; lazima atoe kila kitu cha thamani katika nyumba yake.
32Mtu anayefanya uzinzi hana akili; hufanya hiyo kwa uharibifu wake mwenyewe.
33Anasitahili aibu na majeraha na fedheha yake haiwezi kuondolewa.
34Maana vivu humghadhibisha mtu; hatakuwa na huruma wakati wa kulipa kisasi chake.
35Ujapompa zawadi nyingi, hatakubali mbadala wa kusuruhishwa wala kulipwa.