Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Mithali

Mithali 20

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Divai ni dhihaka na kinywaji kikali ni mgomvi; anayepotea kwa kunywa hana busara.
2Kumwogopa mfalme ni kama kumwogopa simba kijana aungurumaye, yeyote anayemkasirisha hutoa fidia ya maish yake.
3Ni heshima kwa mtu yeyote kujiepusha na mafarakano, bali kila mpumbavu hurukia kwenye mabishano.
4Mtu mvivu halimi majira ya kipupwe; hutafuta mazao wakati wa mavuno lakini hapati kitu.
5Makusudi ndani ya moyo wa mtu ni kama maji yenye kina, bali mtu mwenye ufahamu huyateka.
6Mara nyingi mtu husema yeye ni mwaminifu, lakini ni nani awezaye kumpata yule mwaminifu?
7Mtu atendaye haki hutembea katika uaminifu wake na wana wake wanaofuata baada yake wanafuraha.
8Mfalme anayeketi kwenye kiti cha hukumu akifanya kazi za kuhukumu hupembua kwa macho yake mabaya yote yaliyoko mbele yake.
9Nani anayeweza kusema, “Nimeuweka safi moyo wangu; nipo huru na dhambi zangu”?
10Mizani tofauti na vipimo visivyosawa - Yehova huvichukia vyote.
11Hata kijana hujulikana kwa matendo yake, kwa mwenendo wake kama ni safi na uadilifu.
12Masikio yanayosikia na macho yanayoona- Yehova aliyafanya yote.
13Usipende usingizi au utakuwa masikini; fumbua macho yako na utakuwa na vyakula tele.
14“Mbaya! Mbaya!” anasema mnunuzi, lakini akiondoka anajisifu.
15Ipo dhahabu na mawe ya thamani, lakini midomo yenye maarifa ni kito cha thamani.
16Chukua vazi kama mmiliki wake ataweka fedha kama dhamana kwa deni la mgeni, na lichukue kama anaweka dhamana kwa uzinifu.
17Mkate uliopatikana kwa ulaghai unaladha tamu, lakini baadaye kinywa chake kitajaa kokoto.
18Mipango huimarishwa kwa ushauri na kwa mwongozo wa busara utapigana vita.

19Mmbea hufunua siri na kwa hiyo hupaswi kushirikiana na watu ambao huongea sana.
20Kama mtu atamlaani baba yake au mama yake, taa yake itapulizwa katikati ya giza.
21Urithi uliopatikana mwanzoni kwa haraka utakuwa na mema kidogo mwishoni.
22Usiseme “Mimi nitakulipiza kwa kosa hili” Msubiri Yehova na yeye atakuokoa.
23Yehova huchukia mizani isiyo sawa na vipimo vya udanganyifu si vizuri.
24Hatua za mtu huongozwa na Yehova; namna gani basi ataifahamu njia yake?
25Ni mtego kwa mtu kusema kwa pupa, “Kitu hiki ni kitakatifu” na kuanza kufikiri juu yake kwamba kina maana gani baada ya kufanya kiapo.
26Mfalme mwenye busara huwapepeta waovu na huligeuza juu yao gurudumu la kupuria.
27Roho ya mtu ni taa ya Yehova, hutafiti sehemu zake zote za ndani kabisa.
28Agano la uaminifu na udhamini humhifadhi mfalme; kiti chake cha enzi hufanywa thabiti kwa upendo.
29Utukufu wa watu vijana ni nguvu zao na fahari ya watu wazee ni mvi zao.
30Mapigo yanayoleta kidonda huusafisha ubaya na vichapo hufanya sehemu za ndani kabisa kuwa safi.