Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Mithali

Mithali 9

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Hekima amejenga nyumba yake; amechonga nguzo saba kutoka katika miamba.
2Ameandaa wanyama wake kwa chakula cha usiku; ameichanganya divai yake; na kuandaa meza yake.
3Amewatuma watumishi wake kupeleka mialiko na kutoka mahali pa juu sana kwenye mji anaita:
4“Wale wasiofunzwa waje hapa!” anawaambia wale wasionaufahamu.
5Njoo, ule chakula, na unywe divai nimeshaichanganya.
6Acheni njia zenu za kijinga, na mkaishi; tembeeni katika njia ya ufahamu.
7Yeyote amrekebishaye mwenye dhihaka hukaribisha matusi na yeyote anayemshutumu mtu mbaya atapata madhara.
8Usimshutumu mwenye dhihaka, ama atakuchukia; mshutumu mtu mwenye busara, naye atakupenda.
9Mpe mafundisho mtu mwenye busara, naye atakuwa na busara zaidi; mfundishe mtu mwenye haki, naye ataongeza elimu.
10Hofu ya Mungu ni chanzo cha hekima na maarifa ya Mtakatifu ni ufahamu.
11Maana kwa njia yangu siku zako zitazidishwa na uzima wako utaongezewa miaka.
12Kama unahekima, unahekima kwako mwenyewe, lakini ukidharau, utaibeba peke yako.
13Mwanamke mpumbavu anakelele nyingi- hajafunzwa wala haelewi chochote.
14Anakaa kwenye mlango wa nyumba yake, kwenye kiti cha sehemu ya juu sana ya mji.
15Anawaita kwa sauti wanaopita karibu, watu wale wanaotembea wima katika njia zao.
16Wale ambao hamjafunzwa njoni hapa ndani!” anawaambia wale wasio na akili.
17“Maji ya kuiba ni matamu na mkate unaoliwa kwa siri unapendeza.”
18Lakini hajui kwamba wafu wapo pale, wageni wake wapo kwenye vina vya kuzimu.