Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Mithali

Mithali 28

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Waovu hukimbia wakati hakuna mtu anayewafukuza, bali wale watendao haki ni thabiti kama simba kijana.
2Kwa sababu ya uhalifu wa nchi, kuna wakuu wengi, bali kwa mtu mwenye ufahamu na maarifa, itadumu kwa muda mrefu.
3Mtu masikini mwenye kukandamiza watu wengine masikini ni kama mvua inayopiga ambayo haisazi chakula.
4Wale wanaokataa sheria huwatukuza watu waovu, bali wale wenye kuitunza sheria hupigana dhidi yao.
5Watu wabaya hawafahamu haki, bali wale wanaomtafuta Yehova wanafahamu kila kitu.
6Ni bora mtu masikini ambaye anatembea katika uadilifu, kuliko mtu tajiri ambaye ni mdanganyifu katika njia zake.
7Yeye anayetunza sheria ni mwana mwenye ufahamu, bali mwenye ushirika na walafi humwaibisha baba yake.
8Anayepata mafanikio kwa kutoza riba kubwa anakusanya utajiri wake kwa ajili ya mwingine ambaye atakuwa na huruma kwa watu masikini.
9Kama mtu atageuzia mbali sikio lake kusikia sheria, hata maombi yake ni chukizo.
10Yeye anayempotosha mwenye uadilifu katika njia ya uovu ataangukia kwenye shimo lake mwenyewe, bali wakamilifu watapata urithi mwema.
11Mtu tajiri anaweza kuwa mwenye hekima machoni pake mwenyewe, bali mtu masikini mwenye ufahamu atamtafuta.
12Kunapokuwa na ushindi kwa wenye kutenda haki, kunafuraha kuu, bali wanapoinuka waovu, watu hujificha wenyewe.
13Yeye afichaye dhambi zake hatafanikiwa, bali mwenye kutubu na kuziacha ataonyeshwa rehema.
14Anafuraha ambaye huishi kwa unyenyekevu, bali anayeufanya moyo wake ataanguka katika taabu.
15Kama simba anayeunguruma au dubu anayeshabulia ni kama mtawala mwovu juu ya watu masikini.
16Mtawala anayekosa ufahamu ni mkandamizaji katili, bali mwenye kuchukia aibu atadumu katika siku zake.
17Kama mtu anahatia kwa sababu amemwaga damu ya mtu, atakuwa mkimbizi hadi kifo na hakuna atakayemsaidia.
18Mwenye kuenenda kwa ukaminifu atakuwa salama, bali mwenye njia ya udanganyifu ataanguka ghafla.

19Anayefanya kazi kwenye shamba lake atapata chakula kingi, bali afuataye shughuli za upuuzi atapata umasikini mkubwa.
20Mtu mwaminifu atapata baraka nyingi bali apataye utajiri wa haraka hawezi kukosa adhabu.
21Siyo vema kuonyesha upendeleo, lakini kwa kipande cha mkate mtu atafanya ubaya.
22Mtu mchoyo huharakisha kwenye utajiri, lakini hajui ni umasikini gani utakuja juu yake.
23Anayemkaripia mtu baadaye atapata fadhila zaidi kutoka kwake kuliko mwenye kumsifia sana kwa ulimi wake.
24Yule anayemwibia baba yake na mama yake na kusema, “Hiyo siyo dhambi,” ni mshirika wa mwenye kuharibu.
25Mtu mwenye tamaa huchochea mafarakano, bali anayemtumaini Yehova atafanikiwa.
26Yule anayeutumaini moyo wake mwenyewe ni mpumbavu, bali anayekwenda kwa hekima atajilinda mbali na hatari.
27Mwenye kuwapa masikini hatapungukiwa kitu, bali anayewafumbia macho atapokea laana nyingi.
28Watu waovu wanapoinuka, watu hujificha wenyewe, lakini watu waovu wataangamia, wale watendao haki wataongezeka.