Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Mithali

Mithali 26

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Kama theluji wakati wa joto au mvua kwenye mavuno, ndivyo mpumbavu asivyostahili heshima.
2Kama shorowanda hurukaruka na kumeza wadudu wakati wa kuruka, ndivyo ilivyo laana isiyostahili haishuki.
3Mjeledi ni kwa ajili ya farasi, hatamu kwa ajili ya punda na fimbo ni kwa ajili mgongo wa wapumbavu.
4Usimjibu mpumbavu na kujiunga katika upumbavu wake, au utakuwa kama yeye.
5Mjibu mpumbavu na jiunge katika upumbavu wake, ili asiweze kuwa na busara katika macho yake mwenyewe.
6Anayetuma ujumbe kwa mkono wa mpumbavu huikata miguu yake mwenyewe na kunywa vurugu.
7Miguu ya kiwete inayoning'ia chini ni kama mithali kwenye kinywa cha wapumbavu.
8Kujaribisha jiwe kwenye kombeo ni sawa na kumpa heshima mpumbavu.
9Mwiba unaochoma kwenye mkono wa mlevi ni kama mithali kwenye kinywa cha wapumbavu.
10Mpiga mishale anayejeruhi kila mtu ni kama mtu anayemwajiri mpumbavu au kila mtu anayepita karibu yake.
11Kama mbwa anavyorudia matapishi yake, ndivyo alivyo mpumbavu anayerudia upuuzi wake.
12Je unamwona mtu mwenye busara katika macho yake mwenyewe? Mpumbavu anamatumaini zaidi kuliko yeye.
13Mtu mvivu husema “Kuna simba kwenye barabara! Kuna simba katikati ya njia kuu!”
14Kama mlango unavyogeuka kwenye bawaba zake, ndivyo alivyo mtu mvivu kwenye kitanda chake.
15Mtu mvivu hutia mkono wake kwenye sufuria na bado hana nguvu kuunyanyua kwenda kwenye kinywa chake.
16Mtu mvivu ni mwenye hekima kwenye macho yake mwenyewe kuliko watu saba wenye ufahamu.
17Kama mtu anayeshikilia masikio ya mbwa, ndivyo alivyo mpitajia anayepata hasira kwenye ugomvi ambao si wake.
18Kama mtu mwendawazimu anayetupa mishale,

19ndivyo alivyo ambaye humdanganya jirani yake na kusema, “Je sikuwa naongea utani?”
20Kwa kukosa kuni, moto huzimika; na pale pasipo na mmbea ugomvi hukoma.
21Mkaa ni kwa kuwasha makaa na kuni kwa ajili ya moto, ndivyo alivyo mtu mgomvi kwa kuwasha ugomvi.
22Maneno ya mmbea ni kama chembe tamu; nazo zinashuka chini kwenye sehemu za ndani ya mwili.
23Kioo kinachofunika chombo cha udongo ni kama midomo inayoungua na moyo mbaya.
24Yule ambaye huwachukia wengine huficha hisia zake kwa midomo na hufunika uongo ndani yake mwenyewe.
25Ataongea kwa huruma, lakini usimwamini, maana kuna machukizo saba kwenye moyo wake.
26Ingawa chuki zake zimefunikwa kwa udanganyifu, uovu wake utakuwa wazi katika kusanyiko.
27Anayechimba shimo atatumbukia ndani yake na jiwe litamsaga yule anayelisukuma.
28Ulimi wa uongo huchukia watu unaowajeruhi na kinywa cha uongo husogeza karibu uharibifu.