Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Mithali

Mithali 23

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Unapoketi kula pamoja na mtawala, angalia kwa uangalifu kilichopo mbele yako,
2na kama ni mtu unayependa kula chakula sana weka kisu kooni.
3Usitamani vinono vyake maana ni chakula cha uongo.
4Usifanye kazi sana ili kupata mali; uwe na busara ya kutosha ili ujue wakati wa kuacha.
5Je utaruhusu macho yako yaangaze juu yake? Itaondoka, maana itawaa mabawa kama tai na kuruka angani.
6Usile chakula cha yule mwenye jicho baya- na usiwe na shauku ya vinono vyake,
7maana ni mtu mwenye kuhesabu gharama ya chakula. “Kula na kunywa!” anakuambia, lakini moyo wake haupo pamoja nawe.
8Utatapika kiasi kidogo ulichokula na utakuwa umepoteza sifa zako njema.
9Usiongee katika usikivu wa mpumbavu, maana atadharau hekima ya maneno yako.
10Usihamishe jiwe la mpaka wa kale au kunyang'anya mashamba ya yatima,
11maana Mkombozi wao ni imara na atatetea kesi yao dhidi yako.
12Elekeza moyo wako katika mafundisho na masikio yako kwenye maneno ya maarifa.
13Usizuie kuadilisha mtoto, maana ukimchapa kwa fimbo, hatakufa.
14Ni wewe unayepaswa kumchapa kwa fimbo na kuikoa nafsi yake kuzimu.
15Mwanangu, kama moyo wako una busara, basi moyo wangu utafurahi pia;
16sehemu zangu ndani kabisa zitafurahi sana midomo yako inaponena haki.
17Usiruhusu moyo wako kuwahusudu wenye dhambi, lakini endelea kumcha Yehova siku zote.
18Hakika tumaini lako halitaondolewa na siku zako za hapo baadaye.

19Sikia- wewe! - mwanangu, na uwe mwenye busara na uelekeze moyo wako katika njia.
20Usishirikiane pamoja na walevi, au pamoja na walaji wa nyama walafi,
21maana mlevi na mlafi wanakuwa masikini na usingizi utawavika kwa matambara.
22Msikilize baba yako ambaye alikuzaa na usimdharau mama yako wakati akiwa mzee.
23Inunue kweli, lakini usiiuze; nunua hekima, nidhamu, na ufahamu.
24Baba yake mwenye haki atafurahia sana, na yule amzaaye mtoto mwenye busara atamfurahia.
25Mfurahishe baba yako na mama yako na yule aliyekuzaa afurahie.
26Mwanangu, nipe moyo wako na macho yako yachunguze njia zangu.
27Maana malaya ni shimo refu, na mke wa mume mwingine ni kisima chembamba.
28Anavizia kama mnyang'anyi na huongeza idadi ya wadanganyifu miongoni mwa wanadamu.
29Nani mwenye taabu? Nani mwenye huzuni? Nani mwenye mapigano? Nani mwenye malalamiko? Nani mwenye majeraha bila sababu? Nani mwenye macho mekundu?
30Ni wale ambao huzengea kwenye mvinyo, wale wanaojaribu kuchanganya mvinyo.
31Usiutazame mvinyo ukiwa mwekundu, wakati unametameta kwenye kikombe na kutelemka kwa uraini.
32Mwisho wake unauma kama nyoka na sumu yake kama kifutu.
33Macho yako yataona vitu vigeni na moyo wako utatamka vitu vya ukaidi.
34Utakuwa kama anayelala kwenye bahari au anayelala juu ya mlingoti.
35“Wamenipiga,” utasema, “lakini sikuumia. Wamenichapa, lakini sikuwa na hisia. Nitaamka lini? Nitatafuta kinywaji kingine.”