Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Mithali

Mithali 7

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Mwanangu, yatunze maneno yangu na ndani yako udhihifadhi amri zangu.
2Uzilinde amri zangu ili uishi na uyatunzetu mafundisho yangu kama mboni ya jicho.
3Uyafunge katika vidole vyako; uyaandike katika kibao cha moyo wako.
4Mwambie hekima, “wewe ni dada yangu,” na ufahamu mwite jamaa yako,
5ili ujitunze mwenyewe dhidi ya mwanake haramu, dhidi ya mwanamke mgeni mwenye maneno laini.
6Nilikuwa naangalia kwenye wavu wa dirisha la nyumba yangu.
7Nikawatazama watu mwenye ukosefu wa uzoefu, na miongoni mwa watu vijana nikamwona kijana asiye na akili.
8Kijana huyo alishuka mtaani kwenye kona karibu na yule mwanamke, akaenda kwenye nyumba yake.
9Ilikuwa katika utusiutusi wa siku muda wa jioni, wakati wa usiku na giza.
10Akakutana na yule mwanake, amevaa kama kahaba, katika moyo wa udanyanyifu.
11Alikuwa na kelele na upotovu; miguu yake haikutulia kwenye masikani.
12Alielekea mitaani, kisha sehemu ya sokoni, na katika kila upande alisubiri kwa kuviza.
13Basi akamshika na kumbusu, kwa uso wa nguvu akamwambia,
14leo nimetoa sadaka yangu ya amani, nimelipa nadhili yangu,
15hivyo nilikuja kukutana nawe, kuutafuta uso wako kwa hamu, na sasa nimekupata.
16Nimeweka matandiko juu ya kitanda changu, kitani za rangi kutoka Misri.
17Kitanda changu nimenyunyizia manemane, udi na mdalasini.
18Njoo, tunywe tujishibishe kwa upendo wetu hata asubuhi; tupate furaha kuu kwa matendo ya mahaba.

19Maana mume wangu hayupo nyumbani kwake; amekwenda safari ya mbali.
20Alichukua mkoba wa fedha; atarudi siku ya mwezi mpevu.
21katika maneno yake mengi akamshinda; na kwa midomo yake laini anampotosha.
22Ghafula alimfuata kama maksai anayekwenda kwa mchinjaji, kama ayala aliyekamatwa kwa nguvu,
23mpaka mshale upasue ini lake. Alikuwa kama ndege anayekimbili kwenye mtego. Hakujua kuwa itamgharimu maisha yake.
24Na sasa, wanangu, nisikilizeni; zingatieni maneno ya kinywa changu.
25Moyo wako usiyageukie mapito yake; usipotoshwe katika mapito yake.
26Amesababisha watu wengi kuanguka kwa kuwajeruhi; ameua watu wengi.
27Nyumba yake ipo juu ya barabara ya kwenda kuzimu; huelekea chini kwenye vyumba vya mauti.