Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Mithali

Mithali 2

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Mwanangu, kama ukiyapokea maneno yangu na kuzitunza amri zangu,
2usikilize hekima na utaelekeza moyo wako katika ufahamu.
3kama utalilia ufahamu na kupaza sauti yako kwa ajili ya ufahamu,
4kama utautafuta kama fedha na kupekua ufahamu kama unatafuta hazina iliyojificha,
5ndipo utakapofahamu hofu ya Yehova na utapata maarifa ya Mungu.
6Kwa kuwa Yohova hutoa hekima, katika kinywa chake hutoka maarifa na ufahamu.
7Yeye huhifadhi sauti ya hekima kwa wale wampendezao, yeye ni ngao kwa wale waendao katika uadilifu,
8huongoza katika njia za haki na atalinda njia ya waaminifu kwake.
9Ndipo utakapoelewa wema, haki, usawa na kila njia njema.
10Maana hekima itaingia moyoni mwako na maarifa yataipendeza nafsi yako.
11Busara itakulinda, ufahamu utakuongoza.
12Vitakuokoa kutoka katika njia ya uovu, kutoka kwa wale waongeao mambo potovu.
13Ambao huziacha njia za wema na kutembea katika njia za giza.
14Hufurahia wanapotenda maovu na hupendezwa katika upotovu.
15Hufuata njia za udanganyifu na kwa kutumia ghilba huficha mapito yao.
16Busara na hekima zitakuokoa kutoka kwa mwanamke malaya, kutoka kwa mwanamke anayetafuta visa na mwenye maneno ya kubembeleza.
17Yeye humwacha mwenzi wa ujana wake na kusahau agano la Mungu wake.
18Maana nyumba yake huinama na kufa na mapito yake yatakupeleka kwa wale walioko kaburini.

19Wote waiendeao njia yake hawatarudi tena na wala hawataziona njia za uzima.
20kwa hiyo utatembea katika njia ya watu wema na kufuata njia za wale watendao mema.
21Kwa wale watendao mema watafanya makazi yao katika nchi, na wale wenye uadilifu watadumu katika nchi.
22Lakini waovu wataondolewa katika nchi na wale wasioamini wataondolewa katika nchi.