Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Mithali

Mithali 15

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Jawabu la upole huondoa ghadhabu, bali neno la ukatili huchochea hasira.
2Ulimi wa watu mwenye hekima husifu maarifa, bali kinywa cha wapumbavu humwaga upuuzi.
3Macho ya Yehova yapo kila mahali, yakiwatazama juu ya waovu na wema.
4Ulimi unaoponya ni mti wa uzima, bali ulimi wa udanganyifu huvunja moyo.
5Mpumbavu hudharau marudi ya baba yake, bali yeye anayejifunza kutokana na masahihisho ni mwenye hekima.
6Katika nyumba ya wale watendao haki kuna hazina kubwa, bali mapato ya watu waovu huwapa taabu.
7Midomo ya wenye hekima husambaza maarifa, bali mioyo ya wapumbavu haifanyi hivyo.
8Yehova anachukia sadaka za watu waovu, bali maombi ya watu waadilifu ndiyo furaha yake.
9Yehova anachukia njia ya watu waovu, bali anampenda yule ambaye huandama haki.
10Marudi ya ukatili hungojea kwa yeyote ambaye huiacha njia na yule ambaye huchukia masahihisho atakufa.
11Kuzimu na uharibifu vipo wazi mbele za Yehova; je si zaidi sana mioyo ya wana wa wanadamu?
12Mwenye mzaha huchukia masahihisho; hatakwenda kwa wenye hekima.
13Moyo wenye furaha husababisha uchangamfu wa uso, bali huzuni huvunja moyo.
14Moyo wa mwenye ufahamu hutafuta maarifa, bali kinywa cha wapumbavu hujilisha kwenye upuuzi.
15Siku zote za watu waliokandamizwa ni taabu, bali moyo wenye furaha unakaramu daima.
16Bora kitu kidogo pamoja na kumcha Mungu kuliko hazina kubwa pamoja na ghasia.
17Bora mlo wenye mboga kukiwa na upendo kuliko kuandaliwa ndama aliyenona kwa chuki.
18Mtu mwenye hasira huchochea mabishano, bali mtu ambaye hukawia kukasirika hutuliza ugomvi.

19Mapito ya mtu goigoi ni kama sehemu yenye uwa wa miiba, bali mapito ya mtu mwadilifu ni njia kuu iliyojengwa imara.
20Mwana mwenye busara huleta furaha kwa baba yake, bali mtu mpumbavu humdharau mama yake.
21Upuuzi humfurahia mtu ambaye amepungukiwa akili, bali mwenye ufahamu hutembea katika njia nyofu.
22Mipango huharibika ambapo hakuna ushauri, bali washauri wengi wanafanikiwa.
23Mtu anapata furaha wakati anapotoa jibu la kufaa; je ni zuri kiasi gani neno kwa wakati muafaka!
24Njia ya uzima huwapeleka juu watu wenye hekima, ili waondoke kutoka chini kuzimu.
25Yehova hurarua urithi wa mwenye kiburi, bali huzilinda mali za mjane.
26Yehova huyachukia mawazo ya watu waovu, bali maneno ya upole ni safi.
27Mporaji huleta shida kwenye familia yake, bali yeye ambaye huchukia rushwa ataishi.
28Moyo wa yule atendaye haki hutafakari kabla ya kujibu, bali kinywa cha watu waovu humwanga ubaya wake wote.
29Yehova yupo mbali na watu waovu, bali husikia maombi ya wale watendao haki.
30Nuru ya macho huleta furaha moyoni na habari njema ni afya kwenye mwili.
31Kama utazingatia wakati mtu anapokurekebisha jinsi ya kuishi, utabaki miongoni mwa watu wenye busara.
32Yeye anayekataa karipio hujidharau mwenyewe, bali yule asikilizaye masahihisho hujipatia ufahamu.
33Kumcha Yehova hufundisha hekima na unyenyekevu huja kabla ya heshima.