Text copied!
CopyCompare
Biblia Takatifu - Luka - Luka 1

Luka 1:67-79

Help us?
Click on verse(s) to share them!
67Zakariya, baba yake mtoto, akajazwa Roho Mtakatifu, akatamka ujumbe wa Mungu:
68“Asifiwe Bwana Mungu wa Israeli, kwani amekuja kuwasaidia na kuwakomboa watu wake.
69Ametupatia Mwokozi shujaa, mzawa wa Daudi mtumishi wake.
70Aliahidi hapo kale kwa njia ya manabii wake watakatifu,
71kwamba atatuokoa mikononi mwa adui zetu na kutoka mikononi mwa wote wanaotuchukia.
72Alisema atawahurumia wazee wetu, na kukumbuka agano lake takatifu.
73Kiapo alichomwapia Abrahamu baba yetu, ni kwamba atatujalia sisi
74tukombolewe kutoka adui zetu, tupate kumtumikia bila hofu,
75kwa unyofu na uadilifu mbele yake, siku zote za maisha yetu.
76Nawe mwanangu, utaitwa, nabii wa Mungu Mkuu, utamtangulia Bwana kumtayarishia njia yake;
77kuwatangazia watu kwamba wataokolewa kwa kuondolewa dhambi zao.
78Mungu wetu ni mpole na mwenye huruma. Atasababisha pambazuko angavu la ukombozi litujie kutoka juu,
79na kuwaangazia wote wanaokaa katika giza kuu la kifo, aongoze hatua zetu katika njia ya amani.”

Read Luka 1Luka 1
Compare Luka 1:67-79Luka 1:67-79