Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Luka 1:67-79 in Swahili (individual language)

Help us?

Luka 1:67-79 in Biblia Takatifu

67 Zakariya, baba yake mtoto, akajazwa Roho Mtakatifu, akatamka ujumbe wa Mungu:
68 “Asifiwe Bwana Mungu wa Israeli, kwani amekuja kuwasaidia na kuwakomboa watu wake.
69 Ametupatia Mwokozi shujaa, mzawa wa Daudi mtumishi wake.
70 Aliahidi hapo kale kwa njia ya manabii wake watakatifu,
71 kwamba atatuokoa mikononi mwa adui zetu na kutoka mikononi mwa wote wanaotuchukia.
72 Alisema atawahurumia wazee wetu, na kukumbuka agano lake takatifu.
73 Kiapo alichomwapia Abrahamu baba yetu, ni kwamba atatujalia sisi
74 tukombolewe kutoka adui zetu, tupate kumtumikia bila hofu,
75 kwa unyofu na uadilifu mbele yake, siku zote za maisha yetu.
76 Nawe mwanangu, utaitwa, nabii wa Mungu Mkuu, utamtangulia Bwana kumtayarishia njia yake;
77 kuwatangazia watu kwamba wataokolewa kwa kuondolewa dhambi zao.
78 Mungu wetu ni mpole na mwenye huruma. Atasababisha pambazuko angavu la ukombozi litujie kutoka juu,
79 na kuwaangazia wote wanaokaa katika giza kuu la kifo, aongoze hatua zetu katika njia ya amani.”
Luka 1 in Biblia Takatifu

Luka 1:67-79 in Biblia ya Kiswahili

67 Baba yake Zekaria alijazwa na Roho Mtakatifu na akatoa unabii, akisema,
68 “Asifiwe Bwana, Mungu wa Israeli, kwa sababu amesaidia na alishughulikia wokovu kwa watu wake.
69 Ametuinulia pembe ya wokovu katika nyumba ya mtumishi wake Daudi, kutoka miongoi mwa mwa ukoo wa mtumishi wake Daudi,
70 kama alivyosema kwa kinywa cha manabii wake waliokuweko katika nyakati za kale.
71 Atatuoka kutoka kwa adui zetu na kutoka mikononi mwa wote wanaotuchukia.
72 Atafanya hivi kuonesha rehema kwa baba zetu, na kukumbuka agano lake takatifu,
73 kiapo alichokisema kwa Abrahamu baba yetu.
74 Aliapa kuthibitha kwamba ingewezekana kumtumikia Yeye bila hofu, baada ya kuokolewa kutoka katika mikononi ya adui zetu.
75 katika utakatifu na haki mbele zake siku zetu zote.
76 Ndiyo, na wewe mtoto, utaitwa nabii wa Aliye Juu Sana, kwa kuwa utaenenda mbele za uso wa Bwana ili kumwandalia njia, kuwaandaa watu kwa ajili ya ujio wake,
77 kuwafahamisha watu wake kwamba, wataokolewa kwa njia ya kusamehewa dhambi zao.
78 Hili litatokea kwa sababu ya huruma ya Mungu wetu, sababu ambayo jua tokea juu litatujia,
79 kuangaza kwao wakaao gizani na katika uvuli wa mauti. Atafanya hivi kuiongoza miguu yetu kwenye njia ya amani.”
Luka 1 in Biblia ya Kiswahili