Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - 1 Nyakati

1 Nyakati 6

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Wana wa Levi walikuwa Gerishoni, Kohathi, na Merari.
2Wana wa Kohathi walikuwa Amramu, Izhari, Hebroni, na Uzieli.
3Wana wa Amramu walikuwa Aruni, Musa, Miriamu. Wana wa Aruni walikuwa Nadabu, Abihu, Eleazari, na Ithamari.
4Eleazari akawa baba wa Finehasi, na Finehasi akawa baba wa Abishua.
5Abishua akawa baba wa Buki, na Buki akawa baba wa Uzi.
6Uzi akawa baba wa Zerahia, na Zerahia akawa baba wa Meraioti.
7Meraioti akawa baba wa Amaria, na Amaria akawa baba wa Ahitubi.
8Ahitubi akawa baba wa Zadoki, na Zadoki akawa baba wa Ahimazi.
9Ahimazi akawa baba wa Azaria, na Azaria akawa baba wa Yohanani.
10Yohanani akawa baba wa Azaria, aliye hudumu katika hekalu alilo lijenga Sulemani ndaniya Yerusalemu.
11Azaria akawa baba wa Amaria, na Amaria akawa baba wa Ahitubi.
12Ahitubi akawa baba wa Zadoki, na Zadoki akawa baba wa Shalumu.
13Shalumu akawa baba wa Hilikia, na Hilikia akawa baba wa Azaria.
14Azaria akawa baba Seraia, na Seraia akawa baba wa Yehozadaki.
15Yehozadaki akaenda matekani Yahweh alipo wapeleka utumwani Yuda na Yerusalemu kwa mkono wa Nebukadneza.
16Wana wa Levi walikuwa Gerishomu, Kohathi, na Merari.
17Wana wa Gerishomu walikuwa Libini na Shimei.
18Wana wa Kohathi walikuwa Amramu, Izhari, Hebroni, na Uzieli.

19Wana wa Merari walikuwa Mahili na Mushi. Hawa walikuwa koo za Walawi kwa familia za baba zao.
20Uzao wa Gerishomu ulianza na mwanae Libini. Mwana wa Libini alikuwa Jahathi. Mwanae alikuwa Zima.
21Mwanae alikuwa Yoa. Mwanae alikuwa alikuwa Ido. Mwanae alikuwa Zera. Mwanae alikuwa Yeatherai.
22Uzao wa Kohathi ulianza na mwanae Aminadabu. Mwanae alikuwa Kora. Mwanae alikuwa Asiri.
23Mwanae alikuwa Elikana. Mwanae alikuwa Ebiasa. Mwanae alikuwa Asiri.
24Mwanae alikuwa Tahathi. Mwanae alikuwa Urieli. Mwanae alikuwa uzia. Mwanae alikuwa Shauli.
25Wana wa Elikana walikuwa Amasai, Ahimothi, na Elikana.
26Mwana wa huyu Elikana wa pili alikuwa Zofai. Mwanae alikuwa Nahathi.
27Mwanae alikuwa Eliabu. Mwanae alikuwa Yehoramu. Mwanae alikuwa Elikana.
28Wana wa Samwali walikuwa mzaliwa wa kwanza, Yoeli, na Abija, wa pili.
29Mwana wa Merari alikuwa Mahili. Mwanae alikuwa Libini.
30Mwanae alikuwa Shimei. Mwanae alikuwa Uza. Mwanae alikuwa Shimea. Mwanae alikuwa Hagia. Mwana alikuwa Asaia.
31Haya ndio majina ya wanaume ambao Daudi waliwaeka kusimamia muziki katika nyumba ya Yahweh, baada ya sanduku kuja hapo.
32Walitumika kwa kuimba mbele ya hema, hema la kukutania, mpaka Sulemani alipo jenga nyumba ya Yahweh ndani ya Yerusalemu. Walikamilisha wajibu wao kwa kadiri ya maelekezo waliopewa.
33Hawa walitumika pamoja na wana wao. Katika makabila ya Wakohathi alitoka Hemani mwana muziki. Babu zake walikuwa hawa, kurudi nyuma ya wakati: Hemani alikuwa mwana wa Yoeli. Yoeli alikuwa mwana wa Samweli.
34Samweli alikuwa mwana wa Elikana. Elikana alikuwa mwana wa Yerohamu. Yerohamu alikuwa mwana wa Elieli. Elieli alikuwa mwana wa Toa.
35Toa alikuwa mwana wa Zufi. Zufi alikuwa mwana wa Elikana. Elikana alikuwa mwana wa Mahathi. Mahathi alikuwa mwana wa Amasai. Amasai alikuwa mwana wa Elikana.
36Elikana alikuwa mwana wa Yoeli. Yoeli alikuwa mwana wa Azaria. Azaria alikuwa mwana wa Zefania.

37Zefania alikuwa mwana wa Tahathi. Tahathi alikuwa mwana wa Asiri. Asiri alikuwa mwana wa Ebiasa. Ebiasa alikuwa mwana wa Kora.
38Kora alikuwa mwana wa Izhari. Izhari alikuwa mwana wa Kohathi. Kohathi alikuwa mwana wa Levi. Levi alikuwa mwana wa Israeli.
39Msaidizi wa Hemani alikuwa Asafu, aliye simama mkono wake wa kuume. Asafu alikuwa mwana Berekia. Berekia alikuwa mwana wa Shimea.
40Shimea alikuwa mwana Mikaeli. Mikaeli alikuwa mwana wa Baaseia. Baaseia alikuwa mwana wa Malikiya.
41Malikiya alikuwa mwana wa Ethini. Ethini alikuwa mwana wa Zera. Zera alikuwa mwana wa Adaia.
42Adaia alikuwa mwana wa Ethani. Ethani alikuwa mwana wa Zima. Zima alikuwa mwana wa Shimei.
43Shimei alikuwa mwana wa Yahathi. Yahathi alikuwa mwana wa Gerishomu. Gerishomu alikuwa mwana wa Levi.
44Upande wa mkono wa koshoto wa Hemani walikuwa wasaidizi wake wana wa Merari. Alikuwa Ethani mwana wa Kishi. Kishi alikuwa mwana wa Abdi. Abdi alikuwa mwana wa Maluki.
45Maluki alikuwa mwana wa Hashabia. Hashabia alikuwa mwana wa Amazia. Amazia alikuwa mwana wa Hilikia.
46Hilikia alikuwa mwana wa Amzi. Amzi alikuwa mwana wa Bani. Bani alikuwa mwana wa Shemeri.
47Shemeri alikuwa mwana wa Mahili. Mahili alikuwa mwana wa Mushi. Mushi alikuwa mwana wa Merari. Merari alikuwa mwana wa Levi.
48Walawi, alipangiwa kufanya kazi zote za hema, nyumba ya Mungu.
49Aruni na wana wake walitoa sadaka katika madhabahu kwa ajili ya sadaka za kuteketeza; na sadaka katika madhabahu ya uvumba kwa kazi zote katika pa patakatifu. Hizi sadaka zilifanya maombezi kwa ajili ya Waisraeli, kwa kadiri ya yote ambayo Musa mtumishi wa Mungu aliwaamuru.
50Uzao wa Aruni una kumbukwa kama ifuatavyo: Mwana wa Aruni alikuwa Eleazari. Mwana Eleazari alikuwa Finehasi. Mwana wa Finehasi alikuwa Abishua.
51Mwana wa Abishua alikuwa Buki. Mwana wa Buki alikuwa Uzi. Mwana wa Buki alikuwa Zerahia.
52Mwana wa Zerahia alikuwa Meraiothi. Mwana wa Meraiothi alikuwa Amaria. Mwana wa Amaria alikuwa Ahitubi.
53Mwana wa Ahitubi alikuwa Zadoki. Mwana wa Zadoki alikuwa Ahimazi.
54Hizi ni sehemu ambazo wazao wa Aruni walipangiwa kuishi, wazao wa Aruni ambao walitoka katika koo za Wakohathi (maeneo ya kwanza yalikuwa yao).

55Walipewa Hebroni katika nchi ya Yuda na nchi ya malisho,
56lakini maeneo ya mji na vijiji alipewa Kalebu mwana wa Yefune.
57Kwa wazao wa Aruni waliwapa: Hebroni (mji wa makimblio), na Libina pamoja na nchi ya malisho, Yatiri, Eshitemoa pamoja na nchi ya malisho,
58Hileni pamoja na nchi ya malisho, na Debiri pamoja na nchi ya malisho.
59Waliwapa uzao wa Aruni: Ashani pamoja na nchi ya malisho na Bethi Shemeshi pamoja na nchi ya malisho;
60na kutoka katika kabila la Benjamini walipewa Geba pamoja na nchi ya malisho, Alemethi pamoja na nchi ya malisho, na Anothothi na nchi ya malisho. Jumla ya miji yao ilikuwa kumi na tatu.
61Uzao mwengine wa Kohathi waliwapa kwa sehemu miji kumi kutoka kwa kabila la Manase.
62Kwa uzao wa Gerishomu kwa koo zao tofauti walipewa miji kumi na tatu kutoka kwa makabila ya Isakari, Asheri, Naftali, na nusu ya kabila la Manase huko Bashani.
63Kwa uzao wa Merari walipewa miji kumi, kulingana na koo zao, kutoka kwa makabila ya Rubeni, Gadi, na Zebuluni.
64Hivyo watu wa Israeli walitoa hii miji pamoja na nchi za malisho kwa Walawi.
65Walitoa kwa sehemu miji iliyo tajwa awali kutoka katika kabila la Yuda, Simeoni, na Benjamini.
66Kwa baadhi ya koo za Wakohathi walitoa miji kutoka kwa kabila la Efraimu.
67Waliwapa: Shekemu (mji wa makimbilio) pamoja na nchi ya malisho katika milima ya Efraimu, Gezeri na nchi ya malisho,
68Jokimeamu pamoja na nchi ya malisho, Bethi Horoni pamoja na nchi ya malisho,
69Aiyaloni pamoja na nchi ya malisho, na Gathi Rimoni pamoja na nchi ya malisho.
70Nusu ya kabila la Manase waliwapa Wakohathi: Aneri pamoja na nchi ya malisho na Bileamu pamoja na nchi ya malisho. Hizi zikawa mali za koo za Wakohathi.
71Kwa uzao wa Gerishomu kutoka koo za nusu ya kabila la Manase, waliwapa: Golani huko Baashani na nchi ya malisho na Ashitarothi pamoja na nchi ya malisho.
72Kabila la Isakari liliwapa uzao wa Gerishomu: Kedeshi pamoja na nchi ya malisho, Dabera pamoja na nchi ya malisho,

73Ramothi pamoja na nchi ya malisho, na Anemu pamoja na nchi ya malisho.
74Isakari alipokea kutoka kwa kabila la Asheri: Mashali pamoja na nchi ya malisho, Abdoni pamoja na nchi ya malisho,
75Hukoki pamoja na nchi ya malisho, na Rehobu pamoja na nchi ya malisho.
76Walipokea kutoka kabila la Naftali: Kedeshi iliyo Galileya pamoja na nchi ya malisho, Hamoni pamoja na nchi ya malisho, na Kiriathaimu pamoja na nchi ya malisho.
77Kwa Walawi wengine, uzao wa Merari, walipewa kutoka kabila la Zebuluni: Rimono pamoja na nchi ya malisho na Tabori pamoja na nchi ya malisho.
78Kwa wao pia walipewa, upande wa pili wa Yordani huko Yeriko, kwa upande wa mashariki mwa mto: Bezeri katika jangwa pamoja na nchi ya malisho, Yahzahi pamoja na nchi ya malisho, Kedemothi pamoka na nchi ya malisho, ma Mefathi pamoja na nchi ya malisho. Hizi zilitolewa kutoka kabila la Rubeni.
80Walawi walipokea kutoka kabila la Gadi: Ramothi ya Gileadi pamoja na nchi ya malisho, Mahanaimu pamoja na nchi ya malisho,
81Heshiboni pamoja na nchi ya malisho, na Yazeri pamoja na nchi ya malisho.