Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - 1 Nyakati

1 Nyakati 16

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Wakaleta ndani Sanduku la Mungu na kuweka katika ya hema ambalo Daudi aliandaa. Kisha wakatoa sadaka ya kuteketeza na sadaka ya ushirika mbele ya Mungu.
2Daudi alipo maliza kutoa dhabiu ya kuteketeza na sadaka za ushirika, aliwabariki watu kwa jina la Yahweh.
3Alisambaza kwa kila Misraeli, mwanaume na mwanamke, kipande cha mkate, na kipande cha nyama, na keki ya mzabibu.
4Daudi aliewapangia baadhi ya Walawi kutumika mbele ya sanduku la Yahweh, na kusheherekea, kushukuru na kumsifu Yahweh, Mungu wa Israeli.
5Hawa Walawi walikuwa Asafu kiongozi, wa pili kutoka kwake Zekaria, Yeieli, Shemiramothi, Yehieli, Matithia, Eliabu, Benaia, Obedi Edomu, na Yeieli. Hawa walikuwa wacheze na vyombo vya uzi na vinubi. Asafu alikuwa apige upatu, kwa kelele.
6Benaia na Yahazieli walikuwa wakupiga tarumbeta kila mara, mbele sanduku la agano la Mungu.
7Kisha katika hiyo siku Daudi akawachagua Asafu na kaka zake kuimba hii nyimbo ya shukurani kwa Yahweh.
8Mpeni shukurani Yahweh, liitieni jina lake; fahamisheni mataifa matendo yake.
9Mwiimbieni, imbeni sifa kwake; semeni matendo yake ya ajabu.
10Jisifuni katika jina lake takatifu; mioyo ya wanao mtafuta Yahweh ishangilie.
11Mtafute Yahweh na nguvu zake; tafuteni uwepo wake siku zote.
12Kumbukeni matendo aliyo ya fanya kwenu, miujiza yake na amri za kinywa chake,
13enyi uzao wa Israeli mtumishi wake, enyi watu wa Yakobo, wateule wake.
14Yeye ni Yahweh, Mungu wetu. Amri zake zipo duniani kote.
15Tunzeni agano lake akilini mwenu milele, neno alilo liamuru kwa vizazi elfu moja.
16Anakumbuka agano alilo lifanya na Ibrahimu, na nadhiri yake kwake Isaka.
17Hili ndilo alilo lithibitisha kwa Yakobo kama amri maalumu, na kwa Israeli kama agano la milele.
18Alisema, “Nitakupa nchi ya Kanani kama sehemu ya urithi wako.”

19Nilisema hili mlipo kuwa wachache kwa idadi, wachache sana, mlipo kuwa wageni katika nchi.
20Walienda taifa hadi taifa, kutoka ufalme mmoja hadi mwingine.
21Hakuwaruhusu yeyote awatese; aliwahadhibu wafalme kwa ajili yao.
22Alisema, “Msiwaguse wapakwa mafuta wangu, na msiwadhuru manabii wangu.”
23Imbeni kwa Yahweh, dunia yote; tangazeni wokovu wake siku hadi siku.
24Kirini utukufu wake kwa mataifa, matendo yake makuu kwa mataifa yote.
25Kwa kuwa Yahweh ni mkuu na ni wakusifiwa sana, na ni wakuogopewa kuliko miungu yote.
26Kwa kuwa miungu ya mataifa ni sanamu, lakini ni Yahweh aliye umba mbingu.
27Uzuri wa ajabu na utukufu upo uweponi mwake. Uwezo na furaha upo kwake.
28Mpeni sifa Yahweh, enyi koo za watu, mpeni sifa Yahweh utukufu na uwezo;
29Mpeni Yahweh utukufu upasao jina lake. Leta sadaka na mje kwake. Muinamieni Yahweh katika utakatifu wa uzuri wake.
30Mtetemeke mbele zake, dunia yote. Dunia imeimarishwa; haiwezi kutikisika.
31Mbingu nazo ziwe nafuraha, na dunia ifurahi; na wasema kwa mataifa yote, “Yahweh anatawala.”
32Bahari na ingurume, na inayo ijaza ipige kelele kwa furaha. Mashamba yawe na furaha tele, na vyote vilivyomo ndani yake.
33Na miti iliyopo misituni ipige kelele kwa Yahweh, kwa kuwa anakuja kuhukumu dunia.
34Toeni shukurani kwa Yahweh, kwa kuwa ni mwema, uaminifu wa agano lake la dumu ata milele.
35Kisha sema, “Tuokoe, Mungu wa wokovu wetu. Tukusanye pamoja na utuokoe kutoka kwa mataifa mengine, ilikwamba tutoe shukurani kwa jina lako takatifu na tufurahi katika sifa zako.”
36Na Yahweh, Mungu wa Israeli, asifiwe kutoka milele na milele. Watu wote wakasema, “Amina” na wakamsifu Yahweh.

37Hivyo Daudi akamwacha Asafu na kaka zake pale mbele ya sanduku la Yahweh, kutumika daima mbele ya sanduku, kama kazi za kila siku zilivyo itaji. Obedi Edomu pamoja na ndugu sitini na nane walijumuishwa.
38Obedi Edomu mwana wa Yeduthuni, pamoja na Hosa, walikuwa wawe walinzi wa lango.
39Zadoki kuhani na makuhani wenzake walikuwa watumike mbele ya hema la Yahweh katika mahali pa juu huko Gibeoni.
40Walikuwa watoe sadaka za kuteketeza kwa Yahweh kwenye madhabahu ya sadaka za kuteketeza daima asubui na jioni, kwa mujibu wa yote yalio andikwa katika amri za Yahweh, aliyo wapa Waisraeli kama sheria.
41Hemani na Yeduthuni walikuwa nao, pamoja na walio chaguliwa kwa jina, kumpa shukurani Yahweh, kwasababu uaminifu wa agano lake la dumu ata milele
42Hemani na Yeduthuni walikuwa viongozi wa wao waliopiga tarumbeta, upatu, na vyombo vingine kwa muziki wa kumuabudu Mungu. Wana wa Yeduthuni walilinda lango.
43Kisha watu wote walirudi nyumbani, na Daudi akarudi kubariki nyumba yake.