Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - 1 Nyakati

1 Nyakati 1

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Adamu, Sethi, Enoshi,
2Kenani, Mahalaleli, Yaredi,
3Henoko, Methusela, Lameki.
4Wana wa Nuhu walikuwa ni Shemu, Hamu, na Yafethi.
5Wana wa Yafethi walikuwa ni Gomeri, Magogu, Madai, Yavani, Tubali, Mesheki, na Tirasi.
6Wana wa Gomeri walikuwa Ashkenazi, Rifathi na Togama.
7Wana wa Yavani walikuwa ni Elisha, Tarshishi, Kitimu, na Warodani.
8Wana wa Hamu walikuwa ni Kushi, Misri, Putu, na Kanaani.
9Wana wa Kushi walikuwa ni Seba, Havila, Sabta, Raama, na Sabteka. Wana wa Raama walikuwa ni Sheba na Dedani.
10Kushi akawa baba wa Nimrodi, aliyekuwa shujaa wa Kwanza katika dunia.
11Misri akawa babu wa Waludi, Waanami, Walehabi, Wanaftuhi,
12Wapathrusi, Wakasluhi (Wafilisti walipotoka), na Wakaftori.
13Kanaani akawa baba wa Sidoni, mwanae wa kwanza, na wa Hethi.
14Pia akawa babu wa Myebusi, Mwamori, Mgirgashi,
15Mhivi, Mwarki, Msini,
16Mwarvadi, Msemari, na Mhamathi.
17Wana wa Shemu walikuwa Elamu, Ashuru, Arfaksadi, Ludi, Aramu, Usi, Huli, Getheri, na Mashi.
18Arfaksadi akawa baba wa Sala, na Sala akawa baba wa Eberi.
19Eberi alikuwa na wana wawili wa kiume. Jina la wa kwanza lilikuwa Pelegi, kwa kuwa katika siku zake dunia ilikuwa imegawanyika. Jina la kaka yake lilikuwa Yoktani.
20Yoktani akawa baba wa Almodadi, Shelefu, Hasarmawethi, Yera,
21Hadoramu, Uzali, Dikla,
22Obali, Abimaeli, Sheba,
23Ofiri, Havila, na Yobabu; wote hawa walikuwa uzao wa Yoktani.
24Shemu, Arfaksadi, Sala,
25Eberi, Pelegi, Reu,
26Serugi, Nahori, Tera,
27Abramu, aliye kuwa Ibrahimu.
28Wana wa Ibrahimu walikuwa Isaka na Ishmaeli.
29Hawa ndio wanao: mzaliwa wa kwanza alikuwa ni Nebayothi, kisha Kedari, Abdeeli, Mibsamu,
30Mishma, Duma, Masa, Hadadi, Tema,
31Yeturi, Nafishi, na Kedama. Hawa ndio wana wa Ishamaeli.
32Wana wa Ketura, suria wa Ibrahimu, walikuwa Zimrani, Yokshani, Medani, Midiani, Ishbaki, na Shua. Wana wa Yokshani walikuwa Sheba na Dedani.
33Wana wa Midiani walikuwa Efa, Eferi, Hanoki, Abida, na Eldaa. Wote hawa walikuwa uzaowa Ketura.
34Ibrahimu akawa baba wa Isaka. Wana wa Isaka walikuwa Esau na Israeli.
35Wana wa Esau walikuwa ni Elifazi, Reueli, Yeushi, Yalamu, na Kora.
36Wana wa Elifazi walikuwa ni Temani, Omari, Sefo, Gatamu, Kenazi, Timna, na Amaleki.
37Wana wa Reueli walikuwa ni Nahathi, Zera, Shama, na Miza.
38Wana wa Seiri walikuwa ni Lotani, Shobali, Sebioni, Ana, Dishoni, Eseri, na Dishani.
39Wana wa Lotani walikuwa ni Hori na Hemamu, na Timna alikuwa dada yake Lotani.
40Wana wa Shobali walikuwa ni Alvani, Manahathi, Ebali, Shefo, na Onamu. Wana wa Sebeoni walikuwa ni Aya na Ana.
41Mwana wa Ana alikuwa ni Dishoni. Wana wa Dishoni walikuwa Hemdani, Eshbani, Ithrani, na Kerani.
42Wana wa Eseri walikuwa Bilhani, Zaawani, na Akani. Wana wa Dishani walikuwa Usi na Arani.
43Hawa ndio wafalme walio tawala katika nchi ya Edomu kabla ya mfalme yeyote kuwatawala Waisraeli: Bela mwana wa Beori; na jina la mji wake ulikuwa Dinhaba.
44Bela alipo kufa, Yohabu mwana wa Zera wa Bosra akatawala badala yake.
45Yohabu alipo kufa, Hushamu wa nchi ya Watemani akatawala badala yake.
46Hushamu alipo kufa, Hadadi mwana wa Bedadi, aliye washinda Wamidiani katika uwanja wa Moabu, akatawa badala yake. Jina la mji wake ulikuwa Avithi.
47Hadadi alipo kufa, Samla wa Masreka akatawala badala yake.
48Samla alipo kufa, Shauli wa Rehobothi Hanahari akatawala badala yake.
49Shauli alipo kufa, Baal-Hanani mwana wa Akbori akatawala badala yake.
50Baal-Hanani mwana wa Akbori alipo kufa, Hadari akatawala badala yake. Jina la mji wake ni Pau. Jina la mke wake lilikuwa ni Mehetabeli binti wa Matredi binti wa Mezahabu.
51Hadadi akafa. Wajumbe wa ukoo wa Edomu walikuwa Timna, Alva, Yethethi,
52Oholibama, Ela, Pinoni,
53Kenazi, Temani, Mibsari,
54Magdieli, na Iramu. Hawa ndio walikuwa wajumbe wa ukoo wa Edomu.