1Hawa ndio wana wa Israeli: Reubeni, Simioni, Lawi, Yuda, Isakari, Zebuloni,
2Dani, Yusufu, Benyamini, Naftali, Gadi, na Asheri.
3Wana wa Yuda walikuwa Eri, Onani, na Shela, ambao walizaliwa na binti wa Shua, Wakanaani. Eri, mzaliwa wa kwanza wa Yuda, alikuwa muovu katika macho ya Yahweh, na Yahweh akamwua.
4Tamari, mkwe wake, alimzalia Peresi na Zera. Yuda alikuwa na wana wa kiume wa tano.
5Wana wa Peresi walikuwa Hesroni na Hamuli.
6Wana wa Zera walikuwa Zimri, Ethani, Hemani, Kalikoli na Darda, wote kwa jumla ni watano.
7Mwana wa Karmi alikuwa ni Akani, aliye leta taabu katika Israeli alipo iba kile kilicho hifadhiwa kwa ajili ya Mungu.
8Mwana wa Ethani alikuwa Azaria.
9Wana wa Hezroni walikuwa ni Yerameeli, Ramu, na Kalebu.
10Ramu akawa baba wa Aminadabu, na Aminadabu akawa baba wa Nashoni, kiongozi miongoni uzao wa Yuda.
11Nashoni akawa baba wa Salmoni, na Salmon akawa baba wa Boazi.
12Boazi akawa baba wa Obedi, na Obedi akawa baba wa Yese.
13Yese akawa baba wa mzaliwa wake wa kwanza Eliabu, wa pili Abinadabu, wa tatu Shama.
14Nethaneli wa nne, Radai wa tano.
15Ozemu wa sita, na Daudi wa saba.
16Dada zao walikuwa Seruya na Abigaili. Wana wa Seruya walikuwa Abishai, Yoabu, na Asaheli, jumla watatu.
17Abigali akamzaa Amasa, ambaye baba yake alikuwa Yetheri Mwishmaeli.
18Kalebu mwana wa Hesroni akawa baba wa watoto wa Azubu mkewe, na Yeriothi. Wanawe walikuwa Yesheri, Shobabu, na Ardoni.
19Azuba akafa, na Kalebu akamuoa Efrathi, aliye mzalia Huri.
20Huri akawa baba wa Uri, na Uri akawa baba wa Besaleli.
21Baadae Hesroni (alipo kuwa na miaka sitini) akamuoa binti wa Makiri, baba wa Gileadi. Akamzalia Segubu.
22Segubu akawa baba wa Yairi, aliye miliki miji ishirini na mitatu katika nchi ya Gileadi.
23Geshuri na Aramu wakawapokonya miji ya Yairi na Kenathi, pamoja na miji sitini iliyo zunguka. Hawa wakazi wote walikuwa ni uzao wa Makiri, baba wa Gileadi.
24Baada ya kifo cha Hesroni, Kalebu akalala na Efrata, mke wa baba yake Hesroni. Akamzalia Ashuri, baba wa Tekoa.
25Wana wa Yerameeli, mzaliwa wa kwanza wa Hesroni, walikuwa ni Ramu mzaliwa wa kwanza, Buna, Oreni, Ozemu, na Ahiya.
26Yerameeli alikuwa na mke mwingine, Jina lake lilikuwa Atara. Yeye alikuwa mama wa Onamu.
27Wana wa Ramu, mzaliwa wa kwanza wa Yerameeli, walikuwa Maasi, Yamini, na Ekeri.
28Wana wa Onamu walikuwa ni Shamai na Yada. Wana wa Shamai walikuwa ni Nadabu na Abishuri.
29Jina la mke wa Abishuri lilikuwa Abihaili, na akamzalia Abani na Molidi.
30Wana wa Nadabu walikuwa Seledi na Apaimu, lakini Seledi alikufa pasipo watoto.
31Mwana wa Apaimu alikuwa Ishi. Mwana wa Ishi alikuwa Sheshani. Mwana wa Sheshani alikuwa Alai.
32Wana wa Yada, kaka yake Shamai, walikuwa Yetheri na Yonathani. Yetheri alikufa pasipo mtoto.
33Wana wa Yonathani walikuwa Pelethi na Zaza. Hawa ndio uzao wa Yerameeli.
34Sasa Sheshani hakuwa na watoto wa kiume, bali wa kike pekee. Sheshani alikuwa na mtumishi, wa Kimisri, ambaye jina lake lilikuwa Yariha.
35Sheshani alimkabidhi binti yake kwa Yariha mtumishi wake kama mke wake. Akamzalia Atai.
36Atai akawa baba wa Nathani, na Nathani akawa baba wa Zabadi.
37Zabadi akawa baba wa Efalali, na Afalali akawa baba wa Obedi.
38Obedi akawa baba wa Yehu, na Yehu akawa baba wa Azaria.
39Azaria akawa baba wa Helesi, na Helesi akawa baba wa Eleasa.
40Eleasa akawa baba wa Sismai, na Sismai akawa baba wa Shalumu.
41Shalumu akawa baba wa Yekamia, na Yekamia akawa baba wa Elishama.
42Wana wa Kalebu, kaka yake Yerameeli, walikuwa ni Mesha mzaliwa wake wa kwanza, aliye kuwa baba wa Zifu. Mwanae wa pili, Maresha, allikuwa baba wa Hebroni.
43Wana wa Hebroni walikuwa Kora, Tapua, Rekemu, na Shema.
44Shema akawa baba wa Rahamu, baba wa Yorkeamu. Rekemu akawa baba wa Shamai.
45Mwana wa Shamai alikuwa Maoni, na Maoni alikuwa baba wa Bethsuri.
46Efa, suria wa Kalebu, alimza Harani, Mosa, na Gazezi. Harani akawa baba wa Gazezi.
47Wana wa Yadai walikuwa Regemu, Yothamu, Geshani, Peleti, Efa, na Shaafa.
48Maaka, suria wa Kalebu, alimza Sheberi na Tirhana.
49Pia akamza Shaafu baba wa Madmana, Sheva baba wa Makbena na baba wa Gibea. Binti wa Kalebu alikuwa Aksa. Hawa walikuwa uzao wa Kalebu.
50Hawa walikuwa wana wa Huri, mzaliwa wake wa kwanza kwa Efratha: Shobali baba wa Kiriath-Yearimu.
51Salma baba wa Bethlehemu, na Harefu baba wa Beth-gaderi.
52Shobali baba wa kiriath-Yearimu alikuwa na uzao: Haroe, nusu ya watu Wamenuthite,
53na ukoo wa Kiriath-Yearimu: Waithri, Waputhi, Washumathi, na Wamishrai. Wasorathi na Waeshtaoli walitoka huku.
54Ukoo wa Salma ulikuwa kama ufatao: Bethlehemu, Wanetofathi, Atroth-Beth-Yoabu, na nusu ya Wamenuhothi na Wazori,
55ukoo wa waandishi walio ishi Yabesi: Watirathi, Washimeathi, na Wasukathi. Hawa walikuwa Wakeni walio toka katika uzao wa Hamathi, babu wa Warekabu.