Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - 1 Nyakati

1 Nyakati 25

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Daudi na viongozi wa wafanyakazi wa hema la kuabudia walichaguliwa kwa kazi baadhi walikuwa wana wa Asafu, Hemani, na Yeduthuni. Wanaume hawa walitabiri kwa vinubi, vifaa vya uzi, na upatu. Hii ni orodha ya wanaume walioifanya hii kazi:
2Kutoka wana wa Asafu: Zakuri, Yosefu, Nethania, na Asharela, wana wa Asafu, chini ya mwongozo wa Asafu, ambaye alitabiri chini ya uwangalizi wa mfalme.
3Kutoka wana wa Yeduthuni: Gedalia, Zeri, Yeshaia, Shimei, Hashabia, na Matithia, sita kwa ujumla, chini ya mwongozo wa baba yao Yeduthuni, ambaye alipiga kinubi kwa kutoa shukurani na kumsifu Yahweh.
4Kutoka wana wa Hemani: Bukia, Matania, Uzieli, Shebueli, na yerimothi, Hanania, Hanani, Eliatha, Gidalti, Romamti Ezeri, yoshibekasha, Mallothi, Hothiri, na Mahaziothi.
5Hawa wote walikuwa wana wa Hemani mfalme wa manabii. Mungu alimpa Hemani wana kumi na nne na mabinti watatu kwa ajili ya kumpa heshima.
6Hawa wote walikuwa chini ya mwongozo wa baba yao. Walikuwa ni waimbaji katika nyumba ya Yahweh, pamoja na upatu na vifaa vya uzi walivyohudumu katika nyumba ya Mungu. Asafu, Yeduthuni, na Hemani walikuwa chini ya uwangalizi wa mfalme.
7Wao na kaka zao walikuwa na uwelewa na walifundishwa kutengeneza muziki kwa Yahweh walikuwa na idadi ya 288.
8Walirusha kura kwa majukumu yao, wote sawa, sawa kwa vijana na kwa wazee, kwa walimua na kwa wanafunzi.
9Sasa kuhusu wana wa Asafu: kura ya kwanza iliangukia katika familia ya Yusufu; ya pili iliangukia katika familia ya Gedalia, idadi ya watu kumi na mbili;
10ya tatu iliangukia kwa Zakuri, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;
11ya nne iliangukia kwa Izri, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;
12ya tano iliangukia kwa Nethania, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;
13ya sita iliangukia kwa Bukia, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;
14ya saba iliangukia kwa Yesharela, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;
15ya nane iliangukia kwa Yeshaia, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;
16ya tisa iliangukia kwa Matania, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;
17ya kumi iliangukia kwa Shimei, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;
18ya kumi na moja iliangukia kwa Azareli, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;

19ya kumi na mbili iliangukia kwa Hashabia, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;
20ya kumi na tatu iliangukia kwa Shubaeli, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;
21ya kumi na nne iliangukia kwa Matithia, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;
22ya kumi na tano iliangukia kwa Yeromothi, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;
23ya kumi na sita iliangukia kwa Hanania, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;
24ya kumi na saba iliangukia kwa Yoshibekasha, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;
25ya kumi na nane iliangukia kwa Hanani, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;
26ya kumi na tisa iliangukia kwa Malothi, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;
27ya ishirini iliangukia kwa Eliatha, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;
28ya ishirini na moja iliangukia kwa Hothiri, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;
29ya ishirini na mbili iliangukia kwa Gidalti, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;
30ya ishirini na tatu iliangukia kwa Mahaziothi, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;
31ya ishirini na nne iliangukia kwa Romamti Eza, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili.