Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - 1 Nyakati

1 Nyakati 3

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Sasa hawa ndio wana wa Daudi waliozaliwa kwake huko Hebroni: mzaliwa wa kwanza alikuwa Amnoni, kwa Ahinoamu kutoka Yezreeli; wa pili alikuwa Danieli, kwa Abigaili kutoka Karmeli;
2watatu alikuwa Absalomu, ambaye mama yake alikuwa ni Maaka, binti wa Talmai mfalme wa Geshuri. Wanne alikuwa ni Adoniya mwana wa Hagithi;
3watano alikuwa ni Shefatia kwa Abitali, wasita alikuwa ni Ithraeamu kwa Egla mkewe.
4Hawa sita walizaliwa kwa Daudi huko Hebroni, alipo tawala miaka saba na miezi sita. Kisha akatawala miaka thelathini na mitatu huko Yerusalemu.
5Hawa wana wa nne, kwa Bathshua binti wa Amieli, walizaliwa kwake huko Yerusalemu: Shamua, Nathani, na Sulemani.
6Wana tisa wengine wa Daudi walikuwa ni: Ibhari, Elishua, Elipeleti,
7Noga, Nefegi, Yafia,
8Elishama, na Elifeleti.
9Hawa walikuwa wana wa Daudi, pasipo kuwehesababu wana wa masuria wake. Tamari alikuwa dada yao.
10Mwana wa Sulemani alikuwa ni Rehoboamu. Mwana wa Rehoboamu alikuwa Abiya. Mwana wa Abiya alikuwa Asa. Mwana wa Asa alikuwa Yehoshafati.
11Mwana wa Yehoshafati alikuwa Yoramu. Mwana wa Yoramu alikuwa Ahazia. Mwana wa Ahazia alikuwa Yoashi.
12Mwana wa Yoashi alikuwa Amazia. Mwana wa Amazia alikuwa Azaria. Mwana wa Azaria alikuwa Yothamu.
13Mwana wa Yothamu alikuwa Ahazi. Mwana wa Ahazi alikuwa Hezekia. Mwana wa Hezekia alikuwa Manase.
14Mwana wa Manase alikuwa Amoni. Mwana wa Amoni alikuwa Yosia.
15Wana wa Yosia aliyekuwa mzaliwa wake wa kwanza ni Yohana, wapili Yehoyakimu, mwanae watatu Sedekia, na mwanae wanne Shalumu.
16Wana wa Yehoyakimu walikuwa Yehoyakini na Sedekia.
17Wana wa YehoYakini, mateka, walikuwa Shealtieli,
18Malkiramu, Pedaya, Shenezari, Yekamia, Hoshama, na Nedabia.

19Wana wa Pedaya walikuwa Zerubabeli na Shimei. Wana wa Zerubabeli walikuwa Meshulamu na Hanania; Shelomithi alikuwa dada yao.
20Wanae watano walikuwa Hashuba, Oheli, Berekia, Hasadia, na Yushabu Hesedi.
21Wana wa Hanania walikuwa Pelatia na Yeshaya. Mwanawe alikuwa Refaya, na uzao wake zaidi walikuwa ni Arnani, Obadia, na Shekania.
22Mwana wa Shekania alikuwa Shemaya. Wana wa Shemaya walikuwa Hatushi, Igali, Baria, Nearia, na Shafati.
23Wana watatu wa Nearia walikuwa Elioenai, Hizekia, na Azrikamu.
24Wana saba wa Elioenai walikuwa Hodavia, Eliashibu, Pelaya, Akubu, Yohana, Delaya, na Anani.