Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - 1 Nyakati

1 Nyakati 10

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Wafilisti wakapigana dhidi ya Israeli. Kila mwanaume wa Israeli alikimbia Wafilisti na kuanguka na kufa katika Mlima Giliboa.
2Wafilisti waliwakimbiza Sauli na mwanae. Waflisti walimuua Yonathani, Abinadabu, na Malichishua, wana wake.
3Pambano lilikuwa zito kwa Sauli, na wapiga mishale wakamshambulia. Alipatwa na maumivu makali sababu ya wapiga mishale.
4Kisha Sauli akasema kwa mbeba ngao wake, “Vuta upanga wako na unichome nao. Lasihivyo, hawa wasio tahiriwa watukuja na kunitesa”. Lakini mbeba ngao wake hakutaka, kwa kuwa aliogopa sana. Kwa hiyo Sauli akachukuwa upanga wake na kuuangukia.
5Mbeba ngao alivyoona kuwa Sauli amekufa, naye akaangukia upanga wake na kufa.
6Kwaiyo Sauli akafa, na wana wake watatu, wote wa nyumba yake wakafa pamoja.
7Kila mwanaume wa Israeli katika bonde alivyoona kuwa wamekimbia, na Sauli na wana wake wamekufa, walitelekeza miji yao na kukimbia. Kisha Wafilisti wakaja na kuishi humo.
8Ikawa siku inayofuata, Wafilisti walipo kuja kukagua wafu, walimkuta Sauli na wana wake wameanguka katika Mlima Giliboa.
9Wakamvua nguo zote na kuchukuwa kichwa chake na ngao yake. Wakatuma wajumbe wapeleke habari Filistia yote kwa miungu yao na watu wote.
10Ngao yake wakaeka ndani ya hekalu la miungu yao, na kichwa chake waka kining'iniza katika hekalu la Dagoni.
11Yabeshi Gileadi yote ilipo sikia Wafilisti waliyo mtendea Sauli,
12wanaume wote wa vita wakaenda na kuchukuwa mwili wa Sauli na hiyo ya wanae, na kuirejesha Yabeshi. Walizika mifupa yao chini ya mti huko Yabeshi na wakafunga siku saba.
13Kwaiyo Sauli akafa kwa kuwa hakuwa mwaminifu kwa Yahweh. Hakutii maelekezo ya Yahweh, lakini akauliza ushauri kwa mtu anaye ongea na wafu.
14Hakutafuta mwongozo kwa Yahweh, hivyo Yahweh akamua na kupindua ufalme kwa Daudi mwana wa Yese.