Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - 1 Nyakati

1 Nyakati 22

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Kisha Daudi akasema, “Hapo ndipo nyumba ya Yahweh Mungu itakuwepo, na madhabahu ya sadaka za kuteketezwa za Israeli.”
2Hivyo Daudi akaagiza watumishi wake wawakusanye pamoja wageni wote wanao ishi katika nchi ya Israeli. Aliwapangia kuwa wachonga mawe, kuchonga matofali ya mawe, ilikuweza kujenga nyumba ya Mungu.
3Daudi alisambaza idadi kubwa ya chuma kwa ajili ya misumari na vitasa vya kuweka kwenye malango. Pia alitoa shaba zaidi kushinda kipimo,
4na miti ya mierezi zaidi ya kipimo. (Wasidoni na Watiria walileta mboa nyingi za mierezi kwa Daudi azihesabu.)
5Daudi akasema, “Mwanangu Sulemani ni mdogo na hana uzoefu, na nyumba itayo jengwa kwa Yahweh lazima iwe maridadi, ilikwamba iwe maarufu na ya utukufu kwa nchi zingine. Hivyo nitaanda ujenzi wake.” Hivyo Daudi akafanya maandalizi ya kina kabla ya mauti yake.
6Akaagiza Sulemani mwanae kuitwa na kumuamuru ajenge nyumba ya Yahweh, Mungu wa Israeli.
7Daudi akasema kwa Sulemani, “Mwanangu, ilikuwa dhamira yangu kujenga nyumba mwenyewe, kwa ajili ya jina la Yahweh Mungu wangu.
8Lakini Yahweh alikuja kwangu na kusema, 'Wewe umemwaga damu nyingi na umepigana mapambono mengi. Hauta jenga nyumba kwa jina langu, kwasababu umemwaga damu nyingi kwenye ardhi machoni pangu.
9Walakini, utapata mwana ambaye atakuwa mtu wa amani. Nitampa kupumzika na maadui zake kwa kila upande. Kwa kuwa jina lake litaitwa Sulemani, na nitatoa amani na utulivu kwa Israeli katika siku zake.
10Ata jenga nyumba kwa jina langu. Ata kuwa mwana wangu, na nitakuwa baba yake. Nitaimarisha kiti cha enzi cha ufalme wake juu ya Israeli.
11Sasa, mwanangu, Yahweh awe nawe na kukuwezesha kufanikiwa. Uweze kujenga nyumba ya Yahweh Mungu wako, kama alivyo sema utajenga.
12Yahweh tu akupe uwelewa na ufahamu, ili utii sheria ya Yahweh Mungu wako, ata kapokuweka kiongozi juu ya Israeli.
13Kisha utafanikiwa, kama tu ukitii maagizo na amri Yahweh alizo mpa Musa kuhusu Israeli. Kuwa hodari na mshujaa. Usiogope wala kufadhaika.
14Sasa, ona, kwa bidii kubwa nimeandaa kwa ajili ya nyumba ya Yahweh talanta 100, 000 za dhahabu, talanta milioni moja za fedha, na shaba na chuma katika idadi kubwa. Pia nimetoa mbao na mawe. Lazima uongeze zaidi katika haya.
15Una wafanya kazi wengi: wachonga mawe, maseremala, wanaume wenye ujuzi mbali mbali,
16wenye uwezo wa kufanya kazi na dhahabu, fedha, shaba, na nishati. Hivyo anza kufanya kazi, na Yahweh awe nawe.
17Daudi akawaagiza viongozi wote Waisraeli wamsaidie Sulemani mwanae, akisema,
18“Yahweh Mungu wenu yupo nanyi na amewapa amani kila pande. Amewakabidhi mikononi mwangu wenyeji wote mkoa. Mkoa umetiishwa mbele za Yahweh na watu wake.

19Sasa mtafuteni Yahweh Mungu wenu kwa moyo wenu wote na nafsi. Simameni na mjenge sehemu takatifu ya Yahweh Mungu. Kisha mwaweza kuleta sanduku la agano la Yahweh na vitu vya Mungu ndani ya nyumba iliyo jengwa kwa ajili ya jina la Yahweh.