Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - 1 Nyakati

1 Nyakati 24

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Makundi vya kazi kulingana na uzao wa Aroni yalikuwa haya: Nadabu, Abihu, Eleazari na Ithamari.
2Nadabu na Abihu walikufa kabla ya baba yao kufa. Walikuwa hawana watoto, kwahiyo Eleazari na Ithamari walitumika kama makuhani.
3Daudi pamoja na Zadoki, uzao wa Eleazari, na Ahimeleki, uzao wa Ithamari, waliwagawanya katika makundi yao ya kazi kama makuhani.
4Kulikuwa na wanaume viongozi zaidi kati ya uzao wa Eleazari kuliko kati ya uzao wa Ithamari, kwahiyo waligawanya uzao wa Eleazari katika makundi kumi na sita. Walifanya hivyo na viongozi wa ukoo na uzao wa Ithamari. Magawanyo haya yalikuwa nane kwa idadi, sambamba na koo zao.
5Waliwagawanya bila upendeleo kwa kura, kwa kuwa walikuwa waamuzi watakatifu na waamuzi wa Mungu, kutoka pande zote uzao wa Eleazari na uzao wa Ithamari.
6Shemaia mwana wa Nethaneli mwandishi, Mlawi, aliandika majina yao mbele ya mfalme, muamuzi, kuhani Zadoki, Ahimeleki mwana wa Abiathari, na viongozi wa makuhani na familia za Walawi. Ukoo mmoja ulichaguliwa kwa kura kutoka uzao wa Eleazari, na kisha uliofata utachaguliwa kutoka uzao wa Ithhamari.
7Kura ya kwanza ilienda kwa Yehoiaribu, ya pili kwa Yedaia,
8ya tatu kwa Harimu, ya nne kwa Seorimu,
9ya tano kwa Malikija, ya sita kwa Mijamini,
10ya saba kwa Hakozi, ya nane kwa Abija,
11ya tisa kwa Yeshua, ya kumi kwa Shekania,
12ya kumi na moja kwa Eliashibu, ya kumi na mbili kwa Yakimu,
13ya kumi na tatu kwa Hupa, ya kumi na nne kwa Yesheheabu,
14ya kumi na tano kwa Biliga, ya kumi na sita kwa Imma,
15ya kumi na saba kwa Heziri, ya kumi na nane kwa Hapizezi,
16ya kumi na tisa kwa Pethaia, ya ishirini kwa Yehezikeli,
17ya ishirini na moja kwa Yakini, ya ishirini na mbili kwa Gamuli,
18ya ishirini na tatu kwa Delaia, na ya ishirini na nne kwa Maazia.

19Hii ilikuwa taratibu ya utumishi wao, walipo kuja kwenye nyumba ya Yahweh, wakifuata utaratibu waliopewa na Aruni babu yao, kama Yahweh, Mungu wa Israeli, alivyo waagiza.
20Hawa walikuwa Walawi waliobakia: Wana wa Amiramu, Shebueli; wana wa Shebaeli, Yedeia.
21Wana wa Rehabia: wana wa Rehabia, Ishia kiongozi.
22Wa Waizari, Shelomothi; mwana wa Shelomothi, Yahathi.
23Wana wa Hebroni: Yeria kiongozi, Amaria wapili, Yahazieli watatu, na Yekameamu wanne.
24Wana wa uzao wa Uzieli ulimjumuisha Mika. Uzao wa Mika ulimjumuisha Shamiri.
25Kaka wa Mika alikuwa Ishia. Wana wa Ishia akijumuishwa Zakaria.
26Wana na Merari: Mahli na Mushi. Mwana wa Yaazia, Beno.
27Wana wa Merari: Yaazia, Beno, Shohamu, Zakuri, na Ibrri.
28Wana wa Mahili: eleazari, ambaye alikuwa hana wana.
29Wana wa Kishi: Yerameli
30wana wa Mushi: Mahli, Eda, na yerimothi. Walikuwa walawi, walio orodheshwa na familia zao.
31Wanaume hawa ambao walikuwa vichwa katika nyumba za baba zao na kila wadogo zao, walipiga kura katika uwepo wa Mfalme Daudi, na Zadoki na Ahimeleki, pamoja na viongozi wa familia wa makuhani na Walawi. Walirusha kura kama uzao wa Aroni walivyofanya.