Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Zaburi - Zaburi 9

Zaburi 9:4-17

Help us?
Click on verse(s) to share them!
4Kwa kuwa umenitetea kwa haki; unakaa kwenye kiti chako cha enzi, ukihukumu kwa haki!
5Uliwakemea mataifa; umewaharibu waovu; na kuwa futilia mbali jina lao milele na milele.
6Maadui wamebomoka kama magofu ulipo pindua miji yao. Kumbukumbu yao yote imepotea.
7Bali Yahweh anadumu milele; ameweka kiti chake cha enzi kwa ajili ya haki.
8Naye atauhukumu ulimwengu kwa haki, na atatekeleza hukumu kwa ajili ya mataifa kwa haki.
9Yahweh pia atakuwa ngome kwake aliye onewa, na ngome wakati wa shida.
10Wale wakujuao jina lako wanaamini katika Wewe, kwa ajili yako, Yahweh, usiwaache wale wakutafutao.
11Mwibieni sifa Yahweh, anaye tawala katika Sayuni; waambieni mataifa yale aliyo yatenda.
12Kwa kuwa Mungu alipizae kisasi cha damu hukumbuka; naye hasahau kilio cha anayeonewa.
13Unihurumie, Yahweh; tazama vile ninavyo onewa na wale wanao nichukia, wewe ambaye unaweza kunikwapua katika lango la kifo.
14Oh, ili niweze kutangaza sifa zako. Katika lango la binti sayuni nitaufurahia wokovu wako!
15Mataifa yamedidimia chini katika shimo ambalo walilolitengeneza; miguu yao imenaswa kwenye nyavu walioificha wenyewe.
16Yahweh amejidhihilisha; na kutekeleza hukumu; waovu wameangamia kwa matendo yao wenyewe. Selah
17Waovu wamekataliwa na kupelekwa kuzimu, mataifa yote yanayo msahau Mungu.

Read Zaburi 9Zaburi 9
Compare Zaburi 9:4-17Zaburi 9:4-17