Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Zaburi - Zaburi 99

Zaburi 99:4-9

Help us?
Click on verse(s) to share them!
4Mfalme ana nguvu, naye hupenda haki. Wewe umeimarisha haki; umetenda haki na hukumu katika Yakobo.
5Msifuni Yahwe Mungu wetu na sujuduni miguuni pake. Yeye ni mtakatifu.
6Musa na Haruni walikuwa miongoni mwa makuhani wake, na Samweli alikuwa miongoni mwa wale walio muomba Yeye. Walimuomba Yahwe, naye akawajibu.
7Alizungumza nao toka nguzo ya wingu. Walizishika amri zake takatifu na sheria ambazo aliwapatia.
8Wewe uliwajibu, Yahwe Mungu wetu. Ulikuwa kwao Mungu mwenye kusamehe, lakini uliye adhibu matendo yao ya dhambi.
9Msifuni Yahwe Mungu wetu, na mwabuduni kwenye mlima wake mtakatifu, maana Yahwe Mungu wetu ni Mtakatifu.

Read Zaburi 99Zaburi 99
Compare Zaburi 99:4-9Zaburi 99:4-9