8Mpeni Yahwe utukufu ambao unastahili jina lake. Leteni matoleo na muingie nyuani mwake.
9Mpigieni magoti Yahwe mkiwa mmevaa mavazi ambayo yanaheshimu utakatifu wake. Nchi yote tetemekeni mbele zake.
10Semeni kati ya mataifa, Yahwe anatawala.” Ulimwengu pia umeimarishwa; hauwezi kutikiswa. Yeye huwahukumu watu kwa haki.
11Mbingu na zifurahi, na nchi ishangilie; bahari na ivume na vyote viijazavyo vipige kelele kwa shangwe.