3Bahari zimeinuka, Yahwe; zimemepaza sauti zao; mawimbi ya bahari yapiga ghasia na ngurumo.
4Zaidi ya ghasia ya mawimbi mengi, mawimbi ya bahari yenye nguvu, Yahwe aliye juu ni mwenye nguvu.
5Amri zako makini ni za kuaminika sana; utakatifu huipamba nyumba yako, Yahwe, milele.