5Ni jinsi gani matendo yako ni makuu, Yahwe! mawazo yako ni ya kina.
6Mtu mpumbavu hawezi kuyajua, wala mjinga kuyaelewa haya:
7Wasio haki watakapochipuka kama nyasi, na hata watendao uovu watakapo stawi, bado wataangamizwa kwenye uharibifu wa milele.
8Lakini wewe, Yahwe, utatawala milele.
9Hakika, watazame adui zako, Yahwe! Hakika, watazame adui zako. Wataangamia! Wale wote watendao maovu watatawanywa.
10Wewe umeyainua mapembe yangu kama mapembe ya Nyati wa porini; nimepakwa mafuta safi.