4Yeye atakufunika kwa mbawa zake, na chini ya mbawa zake utapata kimbilio. Uaminifu wake ni ngao na ulinzi.
5Nawe hautaogopeshwa na vitisho wakati wa usiku, wala mishale ipaayo kwa siku,
6wala pigo lizungukalo gizani, wala ugonjwa ujao wakati wa mchana.
7Maelfu waweza kuangukia upande wako na makumi elfu mkono wako wa kuume, lakini uovu hauwezi kukupata.
8Wewe utatazama tu na kuona hukumu ya waovu.
9Kwa kuwa Yahwe ni kimbilio langu! Umfanye Aliye Juu kuwa kimbilio lako pia.
10Hakuna uovu utakao kushinda wewe; mateso hayatakuja karibu na nyumba yako.
11Maana yeye atawaelekeza malaika moja kwa moja kukulinda wewe, na kukuwekea ulinzi katika njia zako zote.