4 Yeye atakufunika kwa mbawa zake, na chini ya mbawa zake utapata kimbilio. Uaminifu wake ni ngao na ulinzi.
5 Nawe hautaogopeshwa na vitisho wakati wa usiku, wala mishale ipaayo kwa siku,
6 wala pigo lizungukalo gizani, wala ugonjwa ujao wakati wa mchana.
7 Maelfu waweza kuangukia upande wako na makumi elfu mkono wako wa kuume, lakini uovu hauwezi kukupata.
8 Wewe utatazama tu na kuona hukumu ya waovu.
9 Kwa kuwa Yahwe ni kimbilio langu! Umfanye Aliye Juu kuwa kimbilio lako pia.
10 Hakuna uovu utakao kushinda wewe; mateso hayatakuja karibu na nyumba yako.
11 Maana yeye atawaelekeza malaika moja kwa moja kukulinda wewe, na kukuwekea ulinzi katika njia zako zote.