2Kabla milima haijaumbwa, wala haujaumba nchi na dunia, tangu milele na milele, wewe ni Mungu.
3Humrudisha mtu mavumbini, na kusema, “Rudi, ewe uzao wa mwanadmu.
4Kwa maana miaka elfu machoni pako ni kama jana ipitapo, na kama saa wakati wa usiku.
5Huwafagia kama vile kwa mafuliko nao hulala; na wakati wa asubuhi wako kama majani yameayo.
6Asubuhi yachipuka na kumea; jioni yakatika na kukauka.
7Hakika, tumeangamizwa kwa hasira yako, na gadhabu yako inatuogopesha sana.